Tazama Video | Download Audio: Walter Chilambo - Siri - Gospo Media
Connect with us

Tazama Video | Download Audio: Walter Chilambo – Siri

Video

Tazama Video | Download Audio: Walter Chilambo – Siri

Shalom mwana wa Mungu! kupitia blog yako pendwa leo tumekusogezea video mpya iitwayo Siri kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania akifahamika kwa jina la Walter Chilambo  video ikiwa imeongozwa na director Crix chini ya usimamizi wa kampuni ya Love Production.

Kupitia video hii mwimbaji Walter Chilambo ameamua kuweka wazi Siri ya mafanikio katika maisha yake kiroho na kimwili mpaka sasa ni kwasababu amekubali kuwa karibu na Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake.

Katika wimbo huu amezungumza mambo kadhaa yanayodhihirisha upendo wake kwa Yesu Kristo licha ya magumu anayopitia ikiwemo kutengwa na kudhihakiwa na watu ambao hawaamini katika wokovu wa damu ya Yesu Kristo hata hivyo Walter Chilambo ameonyesha nguvu ya Imani yake juu ya kumtegemea Yesu pekee kwakuwa anaamini damu yake aliyoimwaga msalabani ndio chanzo cha ukombozi wake kutoka kwenye maisha ya vifungo vya dhambi.

Hii ni moja kati ya kazi nzuri sana zilizoachiwa mwaka huu wa 2017 ikiwa moja ya kazi yenye mafuta ya pekee ya upako wa baraka kwa watu wote wanaohitaji kukombolewa kutoka kwenye vifungo vya dhambi na hakika kupitia muziki huu mzuri utakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako kwakuwa Roho Mtakatifu atakuwa ameshamaliza kazi yake kwako na hii ndio Siri ya mafanikio yako ya Kiroho na Mwili.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kwa moyo wa unyenyekevu kutazama video hii na kupakua wimbo huu wenye mafuta ya baraka yakayokubariki na kukuinua tena kwakuwa Yesu kwetu ndio Siri ya ukombozi wa vifungo vyetu vya dhambi. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na Walter Chilambo wasiliana nae kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 718 069 509
Facebook: Walter Chilambo
Instagram: @walterchilambo
Youtube: Walter Chilambo

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Video

To Top