Video

Tazama Video | Download Audio Music: Mutale Nkonde – Make a Difference

Kutoka nchini zambia mpaka Tanzania leo nimekuwekea video mpya iitwayo ”Make a Difference” (Fanya Tofauti) kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo Injili kutoka nchini humo anayefahamika kwa jina la ”Mutale Nkonde Kapaso” video ikiwa imeongozwa na Brave only Music na wimbo ukiwa umetaayarishwa ndani ya studio za Radio Cafe.

Make a Difference ni wimbo unaolezea nguvu ya Mungu iliyoachiliwa kwa binadamu ili kuleta mabadiliko makubwa katika uso wa dunia na hili linawezekana tu pale ambapo binadamu huyo ataweza kutambua nguvu iliyo ndani yake na kuitumia vile inavyopasa na kuweza kuwabariki wengine. Huu ni wimbo kuhamasisha hasa vijana ambao ndio tegemeo hasa la Mungu katika kuujenga mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Mwimbaji Mutale Nkonde alizaliwa nchini zambia na kuwapoteza wazazi wake akiwa na umri wa miaka 10 na alikutana na Yesu katika mahali ambapo maisha yake yalitawaliwa na ugumu na kuvunjwa sana moyo n kuamua kumkimbilia Yesu kuwa naye karibu kama Baba yake mkuu na mrejeshaji wa huduma yake. Mateso yake yamempa msukumo wa kutoa hamasa kwa watu hasa kupitia nyimbo zake ambazo nyingi zinagusa maisha yake binafsi na anakiri kuwa Baba yake mpendwa Yesu Kristo ambaye kwa huruma yake aliweza kumchukua akiwa hana chochote na kumfanya kuwa kila kitu leo.

Anaamini kuwa kusifu, kuabudu na kueneza ujumbe mzuri wa matumaini ni wito wake, zawadi na shauku kamili iliyo ndani yake katika kuishi ndani ya Yesu na kuwawezesha vijana, watoto na wanawake na kuwahamasisha kuwa kila kitu ambacho Mungu amewaumba kuwa waamini watakua wakithubutu.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utabarikiwa siku ya leo!!

Download Audio

Mitandao ya kijamii:
Facebook: Mutale Nkonde Kapaso
Instagram: @mutale_nkonde
Linkedin: Mutale Nkonde
Twitter: @mutalenkonde
YouTube: Mutale Kapaso

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Christopher Mwahangila - Mungu Hawezi Kukusahau

Next post

Download Audio: GloreySings - I am