Connect with us

Tazama Video | Download Audio: Elizabeth Kasase Feat Mussa Mazingwa – Usikate Tamaa

Muziki

Tazama Video | Download Audio: Elizabeth Kasase Feat Mussa Mazingwa – Usikate Tamaa

Shalom mwana wa Mungu! leo tumekusogezea video mpya iitwayo Usikate Tamaa kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili kutoka mjini Dodoma anayefahamika kwa jina la Elizabeth Kasase akiwa amemshirikisha mwimbaji Mussa Mazingwa, video ikiwa imeongozwa na Director Hassam na audio ikiwa imetayaarishwa ndani ya studio za Adonai chini ya mikono ya prodyuza Raymond.

Hii ni moja kati ya video nzuri sana zenye kubariki na kutia tumaini la imani kwa yeyote anayeitazama video hii ambayo ni hakika imejaa mafunzo ambayo yatakujenga na kukufanya uwe na nguvu zaidi ya kuendelea kumtumaini Yesu Kristo bila kukata tamaa licha ya matatizo uliyonayo au magumu unayopitia.

kupitia video hii mwimbaji Elizabeth anatakumbusha kuwa kitu kizuri katika maisha yetu ni kuwa na Imani thabiti ambayo ndiyo chombo pekee kitakachotuvusha kutoka katika kila gumu tunalopitia na hapo ndipo nguvu za Mungu zinapodhihirika na kutenda makuu kwa yule aliye chini atapelekwa juu na yule aliye kwenye vifungo vya mateso atakombolewa kwa jina la Yesu Kristo Ameen.

Kwa moyo wa unyenyekevu tunakukaribisha kuitazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye ujumbe mzito wa baraka na matumaini na ni hakika utainuliwa sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Elizabeth Kasase kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 759 978 836
Facebook: Elizabeth Kasase
Instagram: @elizabethkasase

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top