Video

Tazama Video | Download Audio: Dee Jones – Nothing Is Impossible

Shalom leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia leo tumekusogezea video ya wimbo wake mpya iitwayo ‘‘Nothing Impossible”(Hakuna Kinachoshindikana) kutoka kwa muimbaji Dee Jones ambaye kwa siku ya leo anasherehekea kuzaliwa kwake, video ikiwa imeongozwa na director Roberto Sandli na kushutiwa huko katika mji Aalesund nchini Norway akiwa na kwaya ya ”Sea Side Soul Teens Choir”.

Dee Jones ni mtayaarishaji, mwandishi na mwimbaji wa kimataifa, ambaye kwasasa anafanya kazi kama director wa muziki katika ziara za muziki kimataifa za muimbaji Sinachi na ameshafanya kazi nyingi za waimbaji wa muziki wa Injili kutoka London na Afrika kusini.

Yeye sasa anafanya kazi kama mkurugenzi wa muziki wa ziara ya Kimataifa ya Sinach. pia amezalisha wasanii wengi na wa kujitegemea katika sehemu mbalimbali duniani – London na Afrika Kusini.

Albamu yake yenye jina la Elevated ilichaguliwa kuingia kwenye tuzo za Best Indie USA katika kipengele cha albamu bora ya mwaka 2011 na pia alishinda tuzo ya ”Star Gospel” mwaka huo huo wa 2011.

Albamu yake mpya ”More Than Music” imeonyesha umahiri wake kama muimbaji wa nyimbo za injili na mtumishi wa Mungu kupitia muziki.

Kwa moyo mkunjufu gospomedia.com tunakukaribisha kutazama video hii na kusikiliza wimbo huu ambao tuna hakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Social Media

Facebook: Dee Jones
Instagram: @deejones

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Music Audio: Evalyne Denis - Nakutamani

Next post

Tazama Video | Download Audio: Sebastian Silas - Moyo Wangu