Connect with us

Tazama Video | Download Audio: Bienvenu Wanzire – Kilichoandikwa

Video

Tazama Video | Download Audio: Bienvenu Wanzire – Kilichoandikwa

Kutoka jijini Dar es salaam leo nimekuwekea video nzuri na yenye kukupa nguvu ya kiroho iitwayo Kilichoandikwa kutoka kwa mtumishi wa Mungu anayefahamika kwa jina la Bienvenu Wanzire, video hii imeongozwa na yeye mwenyewe akiwa ndiye director wa studio yake iitwayo Bienve Production.

Kilichoandikwa ni wimbo unaozungumzia ahadi za Mungu kwa watoto wake, hata kama kuna watu wanakukatisha tamaa juu ya jambo unalolifanya katu usikate tamaa kwakuwa mafanikio yako yapo mikononi mwa Bwana wetu Yesu Kristo hivyo kamwe usiwaangalie wanadamu wanasema nini juu yako, wanafanya nini juu yako katika kukukandamiza na kukuangamiza unachotakiwa kujua ni kwamba Yesu ni mfalme wa ulimwengu na vitu vyote hivyo hakuna mwanadamu atakayeweza kubadilisha neno la Mungu juu ya baraka na ahadi za mafanikio yako juu ya biashara yako, ndoa yako, ajira yako, Elimu Yako, Afya yako na uchumi wako ukiamini hakika Mungu atakutendea.

Hii ni video inayobeba jina la albamu yake mpya anayotayarajia kuiachia mwezi Disemba 2017 itakayopatikana kwenye mfumo wa Audio CD na DVD.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua sana!! Karibu.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Bienvenu Wanzire kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 687 925 538
Facebook: Bienvenu Wanzire
Instagram: @bienvenuwanzire
Twitter: @bienvenuwanzire

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Video

To Top