TAMUFO na NSSF kuwawezesha wanamuziki kiuchumi septemba 2, 2017. - Gospo Media
Connect with us

TAMUFO na NSSF kuwawezesha wanamuziki kiuchumi septemba 2, 2017.

Uncategorized

TAMUFO na NSSF kuwawezesha wanamuziki kiuchumi septemba 2, 2017.

Tanzania Music Foundation (TAMUFO) wakishirikiana na NSSF (Shirika la mfuko wa jamii wa taifa), wanakukaribisha kwenye  mkutano maalumu wa wanamuziki utakaofanyika tarehe 2.09.2017 yaani Jumamosi hii katika ukumbi wa NSSF uliopo Ilala Boma katika Jengo la NSSF Mafao House.

Mgeni rasmi wa mkutano huo anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda.

Akiongea na gospomedia.com mmoja wa waratibu wakuu wa mkutano huu Bi.Stella Joel amesema kuwa huu ni mkutano wa kipekee utakaohusu kufungua fursa mbali mbali za kiuchumi kwa wanamuziki wetu nchini jambo hili limejitokeza mara baada ya taasisi ya TAMUFO kuona wanamuziki mbalimbali nchini wakiwa na changangamoto mbalimbali hasa za kichumi zinasababisha kutofikia matarajio yao ya kimuziki na maisha yao kwa ujumla hali inayopelekea kukata tamaa na vipaji vyao kufa kutokana na kukosa msaada wa kiuchumi na kuzorotesha mwelekeo wa huduma zao kimuziki.

Moja kati ya fursa zinazotarajiwa kutolewa siku hiyo ni pamoja kuwawezesha wanamuziki kupata viwanja, nyumba pamoja na mafao ya Bima ya Afya, Hata hivyo kutakuwa na mambo mengine mengi wa ajili ya kuinua maisha ya wanamuziki kiuchumi. mkutano huu utaanza saa mbili asubuhi na kuendelea, chai na chakula cha mchana vitatolewa bure kabisa na hakutakuwa na kiingilio.

“Nawasihi wanamuziki, waimbaji na wadau wote wa muziki (hasa wa nyimbo za Injili) kufika katika mkutano huu muhimu ili sisi kama TAMUFO tuweze kutimiza kusudi letu la dhati kabisa katika kuinua maisha ya wanamuziki wetu nchini Tunawakaribisha sana. Alisema mratibu huyo.

Kwa maelekezo zaidi juu ya mkutano huu na jinsi ya kufika wasiliana na uongozi wa TAMUFO kupitia:

simu/whatsapp: +255 756 846 166,

 +255 767 127 256, +255 658 277 724.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Uncategorized

To Top