Habari

Tamasha la Mwanamke wa Imani Kufanyika Septemba 17, 2017 Kigamboni.

Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Ritha Komba, anawakaribisha wadau na mashabiki wake wote katika Tamasha lake kubwa na la kipekee linalofahamika kwa jina la ”Mwanamke wa Imani” ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 17 Septemba 2017 katika kituo cha maombezi Eloi Centre kilichopo eneo la kisiwani, Kigamboni kuanzia saa nane mchana na kuendelea.

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Ritha Komba amesema kuwa lengo kuu la Tamasha hilo ni kumtia moyo mwanamke aliyekata tamaa na kuvunjika moyo kutokana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kama wanawake katika maisha yao ya kila siku hasa katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi, ndoa na familia, ajira na mambo mengine mengi hivyo kupitia tamasha hili anaamini litawaleta pamoja na kuwauganisha wanawake hawa kwa kubadilishana mawazo, kutoa shuhuda mbalimbali na kutiana moyo kupitia neno la Mungu litakalotolewa siku hiyo ili kuweza kuinua imani zao.

Tamasha hilo litaongozwa na wanenaji na wahamasishaji mbalimbali walioalikwa siku hiyo ambao ni pamoja na Nabii Angel Richard, Eva Kileo, Dr.Tumaini Msowo, Joyce Ombeni, Neema Walele, huku wakisindikizwa na huduma ya uimbaji kutoka kwa waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam ambao watahudumu siku hiyo ambao ni pamoja na Jessica Bm Honore, Betty Barongo, Rehema Lupilya na wengine Wengi, hivyo mwimbaji Ritha Komba amewasihi wadau na watu wote hasa wanawake na mabinti kufika kwenye tamasha hilo ambalo amethibitisha kuwa litakuwa ni la kipekee katika kuwakomboa wanawake wanaopitia changamoto ambazo kwa namna moja ama nyingine zinawakwamisha kufikia malengo yao.

Mbali ya kuwa mbeba maono wa tamasha hili la ”Mwanamke wa Imani” Ritha Komba ni muimbaji mahiri ambaye kwasasa anatamba na video yake iitwayo ”Kivulini” ikiwa ni moja ya video bora kabisa zilizofanya vizuri mwezi wa sita 2017 kama hujawahi kuitazama tumekuwekea hapa chini uweze kuitazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utabarikiwa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ritha Komba kupitia
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook: Ritha Komba
Instagram: @rithakomba
Youtube: Ritha Komba

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Hizi Ndizo Nyimbo Kumi Bora Zilizofanya Vizuri Mwezi wa Saba 2017. Sikiliza Hapa.

Next post

Tazama Video | Download Audio: Jimmy Gospian - Nimekuona