Connect with us

Tamasha kubwa la Nuru ya Mtaa Kufanyika Tarehe 17.09.2017 Jijini Arusha.

Matukio

Tamasha kubwa la Nuru ya Mtaa Kufanyika Tarehe 17.09.2017 Jijini Arusha.

Kutoka jijini Arusha kundi la waimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa Gospel- HipHop Machalii wa Yesu linawakaribisha wakazi wote wa Arusha na mikoa yote ya jirani kwenye tamasha kubwa la kusifu na kumwabudu Mungu kwa mtindo wa Gospel-Hip Hop linalofahamika kwa jina la “Nuru ya Mtaa”.
Tamasha hili linatrajiwa kufanyika tarehe 17.09.2017 katika ukumbi wa Metropole jijini Arusha kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni kwa kiingilio cha shilingi elfu 3000/- tu.

Tamasha hili litahusisha waimbaji na rapa mbalimbali wa Gospel-HipHop kutoka ndani na nje ya Tanzania, kutoka Kenya atakuwepo Pastor Martin Guya, kutoka Dar es salaam atakuwepo Rungu la Yesu, Elandre na Wanaharakati kutoka Kaskazini(WIKA) ambao wote kwa pamoja watahudumu siku hiyo katika kusifu na kumwabudu Mungu. Usipange kukosa tamasha hili mwana wa Mungu..

Wote mnakaribishwa!

Kwa maelezo zaidi kuhusu tamasha hili wasiliana na uongozi wa Machalii wa Yesu kupitia:

Facebook/Instagram: Machalii wa Yesu

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Matukio

To Top