UncategorizedVideos

Video | Audio: Sunny Praise – You Are Beautiful

Mwimbaji anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini nigeria anayefahamika kwa jina la Sunny Praise leo kwa mara ya kwanza tuaitambulisha kwako video yake mpya iitwayo You Are Beatiful ambapo wimbo huu uliachiwa mwanzoni mwa mwaka 2016 na kufanya vizuri sana chini humo na nje ya mipaka pia. Video hii imeongozwa na director Maurizio Ghiotti na muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Spiritual Beatz chini ya labo yake iitwayo Loveworld Music and Arts.

”You Are Beatiful”(Wewe ni mzuri) ni wimbo wa sifa, kuinua jina la Mungu na kazi zake za kubwa na za ajabu. Wimbo huu ni kwa ajili ya watu wote wanaopenda na kutaka kufanya ibada kwa Mungu na sifa. Video hii imerekodiwa katika sehemu mbalimbali za bara la ulaya ikionyesha ajabu na uzuri wa Mungu kupitia picha nzuri zinazoonesha maeneo ya kushangaza.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu mzuri utakaokuongoza na kukubariki sana. Ameen!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na muimbaji Sunny Praise kupitia
Facebook: Sunny Priase Simu/WhatsApp: +234 8032273040
Instagram: @am_sunnypraise
Twitter : @sunnypraise
Youtube: sunnypraise
Email: sunnypraise1@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Mahakama ya hakimu mkazi yawaondolea zuio viongozi wa EAGT

Next post

Video | Audio: Ivan Mosha - Siku Hazigandi