Mafundisho

SOMO LA FRED MSUNGU: NGUVU ZA KIUME KWA MWANAUME

NGUVU ZA KIUME

1:Nguvu ya Mungu (Matendo 1:8 , waefeso 1:19, waefeso 3:20)

2:Nguvu ya jina. (Mithali 22:1, Mwanzo 12:2-3)

3:Nguvu ya pesa/ucuhumi (muhubiri 10:19)

Kama yapo mambo kwa mwanaume kuyatafuta sana basi ni hayo hapo juu tena kwa mtiririko wake kama ulivyo. Nguvu ya Mungu ni lazima iwe ya kwanza kwa mwanaume, wengi sana wamehangaikia na kutafuta namba 2 na 3, na wakasahau ukipata jina na pesa bila kumpata Mungu umeupata uharibifu. Lakini pia kuna kundi ambao wao hawaamini katika nguvu ya uchumi na wanaamini nguvu ya Mungu lakini cha ajabu wanatawaliwa na kufanyiwa maamuzi yanayoenda kinyume na matakwa ya Mungu na watu waovu wenye nguvu ya Pesa na majina (nafasi).

1: Nguvu ya Mungu ambayo inakua kupitia roho wa Mungu, ambaye Yesu aliahidi kutupa na kabla ya kupokea waliamuliwa kutofanya lolote kwanza mpaka atakapowajia Roho mtakatifu (Nguvu ya Mungu) kwenye kitabu cha ufunuo anaeleza juu ya Roho Saba (7) za Mungu ambazo Isaya anaziweka wazi katika sura ya 11:2

Roho ya bwana
Roho ya hekima
Roho ya ufahamu
Roho wa Ushauri
Roho wa Uweza
Roho ya maarifa
Roho ya kumcha Bwana

Ukiangalia kwa makini hapa utagundua kwanini nguvu ya Mungu inasimama kama kipaumbele nambari 1, Kwa mtiririko wa Roho hizo kama zikifanya kazi ndani yako hakuna namna utakosa yale mawili yaliosalia
1:Jina
2:Pesa

Sasa hapa kama mwanaume wa Ufalme ni vizuri ukitambua namna ya kucheza na kipaumbele nini kinatakiwa kuanza na kwanini…!

Nguvu ya Mungu (Roho Wa Mungu) anapokua juu yako yeye hua sababu ya pesa na jina…kwasababu hekima anapokua juu yako, maarifa na uweza hizo ni nyenzo zitakazokuwezesha kuona hazina zilizofichika na kua na majibu ya maswali ya watu kwenye maeneno mbali mbali (Biashara, uchumi, siasa, mahakamani, kwenye michezo na kila sekta )

Ukishakua jibu kwa maswali ya watu hakuna namna utakosa Umaarufu na Pesa maana wewe ni jibu la swali. Ni vizuri tujue Pesa na Umaarufu (jina) ni matokeo baada ya kazi fulani.
Sasa ujinga ni kutafuta Umaarufu au pesa kabla ya kufanya kazi au kutimiza kusudi, Umaarufu au Pesa havitafutwi kwa mwanaume ..!hua vinakuja kama matokeo baada ya kazi iliyofanyika mahali fulani na kuleta matokeo chanya.

KWANINI NGUVU YA MUNGU IWE KIPAUMBELE NAMBA MOJA (1)?

Ni vizuri sana tujue kwamba tunaishi kwenye ulimwengu ambao kila linalofanyika limepangwa katika ulimwengu wa Roho kulingana na falme husika. usisahau ulimwengu unaongozwa na unaongozwa na falme mbili
1:Ufalme wa nuru
2:Ufalme wa Giza

Sasa tatizo la wanaume wengi wanaojiita wapo katika ufalme wa Mungu wanakosa nguvu ya ufalme huu na bado wanataka kushindana na watu wa mataifa ambao wao wanatumia nguvu ya ziada (Wanawezeshwa na ufalme wao kwa manufaa ya kujenga ufalme wao) Kitu ambacho hakitawezekana. Na ndio maana kumekua na ukomo wa umiliki wa Mali kwa watu wa Mungu maana wamesahau kwamba kuna falme iliyo kinyume chetu na Vita ya kiroho tunapigana kimwili.

Ni vizuri ifike mahali tuelewe hakuna namna mtu atakua tajiri kama hayupo sehemu moja kati ya falme hizi mbili. (namaanisha utajiri) achana na Ile dhana ya kumiliki vigari na ki-ghorofa, hapa naongelea utajiri wa maana.

Mwanaume ili uwe Na uwezo Wakua mfanyabiashara mkubwa, mwanasiasa mwenye hekima, Mchumi, mtu wa maamuzi zaidi ya wale wa ulimwengu huu hakikisha unatafuta hii nguvu ya kwanza ili ikupe msuli wa kupambana na wale wa upande wa pili, Kwa taarifa yako usidhani matajiri wale wako tu kizembe zembe kama wewe wanawezeshwa Na nguvu fulani (mambo ya rohoni) na ndio maana wewe unaetumia nguvu zako unapigana ila kuna mahali unaona kabisa unagonga mwamba. Nakupa maarifa leo swala la umiliki na utawala ni swala la kiroho kuliko unavyoweza kudhani, na vita ya rohoni lazima ipiganwe na watu wa Rohoni tu…..sasa wale wananamna yao ila wewe nimekupa siri leo hebu jaribu kujifungamanisha na nguvu ya Mungu (Roho Mtakatifu) uone kama hautafunuliwa mambo yanayoendelea upande wa pili na ukiitumia kanuni hii ipasavyo kufanikiwa kupita kikomo ni lazima.

NGUVU ZA KIUME

1:MUNGU
2:JINA
3:PESA

FRED MSUNGU

PURE MISSION | +255653318117

(C) 2016

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

MUSIC VIDEO: ADAWNAGE BAND - I LIVE FOR YOU

Paul Clement
Next post

FAHAMU KUHUSU UJIO MPYA WA PAUL CLEMENT NA SIRI YA UKIMYA WAKE