Mafundisho

SOMO LA FRED MSUNGU: MAJIRA, KUSUDI NA UKOMO WAKE SEHEMU YA TATU (B)

NAMNA YA KUKAA KITI CHA PILI KWENYE NAFASI YA KWANZA

Kama ambavyo tuliona katika somo la kwanza hii vita iliyokuwapo baina ya Sauli (mfalme) pamoja na Daudi ambaye Bwana alimpaka mafuta kumuandaa kuwa mfalme, na kabla hatujafika mbali ni vizuri tuelewe kwa mujibu wa maandiko moyo wa Bwana haukuwa radhi tena na sauli kutokana na kwamba alikua ametenda kinyume na mapenzi ya Bwana, na Bwana akampaka Daudi mafuta badala yake… Lakini jambo kubwa la msingi la kujifunza kutoka kwa Daudi ni hili hapa..! Pamoja na kujua haya yote bado alikuwa na subira ya majira yake na bado aliendelea kuiheshimu na kuitambua nafasi ya Sauli kama mfalme na kiongozi kwake

1 SAMWELI 24:5

5 – Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli. 6 – Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.

Daudi alikuwa anajua fika kwamba Bwana amempaka mafuta yeye na amemkataa Sauli, na ukisoma hapo kuanzia mstari wa 5 ni wakati ule Sauli amelala na Daudi akaenda na kukata kipande cha vazi la Sauli, Hii ina maana kwamba kwa mazingira yale Daudi alikua na uwezo, sababu na nafasi ya kumuua Sauli lakini hakufanya hivyo pamoja na kwamba alijua fika Sauli anamtafuta ili amuue .

Kwanini Daudi hakumuua sauli..? (adui yake)

Mstari wa 6 unajibu kwa undani na ufasaha sana swali hili, Unaona hapo Daudi anasema ‘nisimtendee bwana wangu (sauli)”

(a) Bado Sauli alikuwa na mamlaka kwake kama kiongozi

Pamoja na kwamba Sauli alikua ameshaharibu kweli, lakini kwasababu bado Bwana alikuwa hajamtoa kweli ile nafasi Daudi bado alitakiwa kuwajibika kwa sauli kama mtumishi

Bwana wangu -Neno hili linawakilisha heshima au nafasi ya mtu fulani, na Hapa huyu bwana anayemzungumzia Daudi ni Sauli. Ninachojifunza hapa bado Daudi anatii mamlaka iliyopo juu yake hata kama imemtendea sivyo….Hii ni muhimu sana kuijua kwasababu itakupa hatua kubwa sana, Kuna wakati ni kweli viongozi wetu, wachungaji, mabosi wanatukosea sana na wanafanya kwa namna isiyo sawa na kuna wakati unaona kabisa upepo wa ile nafasi unavumia kwako, Pamoja na haya yote kutokea ni muhimu sana uiheshimu nafasi ya yule mtu…ni kweli kakukosea na ni kweli hafanyi sawa lakini kwa nafasi aliyopo kama bado Bwana hajayathibitisha majira ya ukomo wa yule mtu bado unatakiwa kuitambua tu kama mkubwa au kiongozi kwako. Watu wengi wamejikosesha kwenye eneo hili kwa kutumia makosa ya wakubwa au watu waliowekwa juu yao kwa kuwaadhibu au kuwanenea vibaya kwa kisasi, ni vizuri uelewe zipo ngazi kwenye ufalme wa Mungu na yule anayetoa zile ngazi ndiye aliye na jukumu la kuhukumu kwa kila kosa na kila mkosaji.

Baba (kiongozi ) atahukumiwa kwa nafasi yake na mtoto (muongozwa) atahukumiwa kwa nafasi yake kila mmoja kwa jinsi alivyofanya usipo lielewa hili utaanza kusumbuka kutafuta kupigana na kiongozi wako kisa amekukosea wakati nafasi hiyo si yako

(b)Daudi aliitambua nafasi ya Sauli kama mtu aliechaguliwa na Bwana

Ukiendelea kusoma mstari huo huo wa sita utaona Daudi anatoa sababu ya kutomuua Sauli anawaambia watumishi wake na kumtambulisha Sauli kama MASIHI WA BWANA maana ya neno hili ni mpakwa mafuta wa Bwana. Hapa nimepata jambo kubwa sana na la msingi ambalo mimi na wewe tunatakiwa kujifunza.

Anayepaka mafuta watu ni Bwana (Mungu mwenyewe) kama ni hivi basi na mwenye jukumu la kuyaondoa haya mafuta juu ya mtu ni Bwana mwenyewe, sasa haijalishi unaona kwa kiasi gani umekosewa au umedhihirisha kwamba Bwana kakupaka mafuta, Usijihusishe kabisa katika kutaka kumpindua mtu kwenye nafasi aliyopo hata kama yeye anakupiga vita, kama mtu mwenye hekima jitahidi sana kumkwepa na si kutafuta mudhurubau kupigana naye vita , maana kupigana vita na masihi wa Bwana kama Bwana mwenyewe hajaondoa mkono wake juu yake maana yake unapigana vita na Bwana na Biblia inasema washindanao na Bwana watapondwa kabisa

( 1SAMWELI 2:10) Kama unauhakika hiyo nafasi ni Bwana ndie kakupa, acha yeye alikamilishe jambo alilolianza usitake kujifanya unamsaidia Mungu itakula kwako, Ufalme wa Mungu unaendeshwa kwa kanuni za ki Mungu

Majira yako yakifika kwa njia yeyote ile utakalia kiti, hakuna haja ya kuuwahisha wakati acha Mungu wa majira na nyakati ajitetee mwenyewe na atimize alichosema juu yako, Watu wengi wameahidiwa makuu lakini hayakutokea si kwasababu Mungu muongo la hasha! ila ni kwasababu wao wenyewe walizitoa mimba za hatma kwa kukosea kanuni na kutoyasubiri majira sahihi ya Mungu juu ya ahadi yao. Ni kweli mwanamke mwenye mimba hatma au mwisho wake anaoutarajia ni mtoto, lakini huyo mtoto akilazimishwa kuzaliwa kabla ya wakati hataishi..na hii ndio nguvu iliyopo ndani ya MAJIRA.

NINI CHA KUFANYA MTU ALIYEJUU YAKO /KIONGOZI WAKO ANAPOKUKOSEA..?

Baada ya somo lililopita moja ya maswali ninmeulizwa kwa wingi ni hili swali, watu wametamani sana kujua nini cha kufanya .

1SAMWELI 24:11

11 – Tena, baba yangu, tazama, tafadhali, tazama upindo wa vazi lako mkononi mwangu; maana ikiwa nimeukata upindo wa vazi lako, nisikuue, ujue, na kuona ya kuwa hakuna uovu wala kosa mkononi mwangu, wala sikukukosa neno; ingawa wewe unaniwinda roho yangu ili kuikamata. 12 – Bwana atuamue, mimi na wewe, na Bwana anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.

Jibu la swali hili wala halihitaji maelezo mengi, Moyo wa unyenyekevu na kujishusha ndicho kitu ninachokiona kwa Daudi nikisoma mstari wa 12. Kama ambavyo nilisema pale juu kama anaYetoa nafasi ni Bwana na Biblia inamtaja yeye kama hakimu wa haki basi kesi kama hii ikitokea njia ya pekee ni kuacha Bwana aamue mwenyewe.

Ninajua fika huwa si jambo jepesi kuachilia kirahisi na ninajua pia watu wametendewa sivyo na wanamaumivu mazito na uchungu, Lakini si wewe tu ukisoma vizuri mistari ya nyuma kitabu hiki cha 1 Samweli, utaona jinsi ambavyo Daudi alimtumikia Sauli kwa uaminifu na hakuna mahali alimkosea lakini bado Sauli alitaka kumuangamiza, Pamoja na yote haya bado Daudi anasamehe anamuachia Bwana aamue kwa majira yake. Hili ni jambo kuu sana la kujifunza kwamba moyo au sifa ya mtu mkuu wa Mungu kama Daudi ni kusamehe, Hii ni muhimu sana acha Bwana apigane vita yako maana ukitaka kupambana mwenyewe unaweza kuikosa hata hiyo ahadi ambayo umekua ukiingoja kwa muda wa miaka mingi, kumbuka Mungu ni Mungu wa majira kanuni na kusudi zaidi sana ni Mungu wa kutunza agano, kama alisema yapo mambo yako ya kutimiza yafanye hayo na sehemu yake muachie yeye

(KUTOKA 14: 14)

14 – Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

                           MATOKEO

Baada ya mgogoro huu wa muda na vita kubwa baina ya mtu aliyeko kwenye kiti na aliechaguliwa utaona hapa vita iliyokuwa ya silaha na kuwindana kwa vifaa vya kivita Daudi anaishinda kwa neno la hekima. Baada ya kumwambia na kumdhihirishia Sauli jinsi alivyokua na nafasi na uwezo wa kumuua mara kadhaa na hakufanya hivyo, Jambo hili linamgusa na kuleta hukumu ndani ya moyo wa Sauli na hata bila yeye kujijua anajikuta anatoa hukumu ya haki juu yao, na ndivyo ilivyokuwa.

1 Samweli 24 : 17-20

17 – Akamwambia Daudi, Wewe u mwenye haki kuliko mimi; maana wewe umenitendea mema, nami nimekutenda mabaya. 18 – Nawe umeonyesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani Bwana aliponitia mikononi mwako, hukuniua.

19 – Maana mtu akimwona adui yake, je! Atamwacha aende zake salama? Basi Bwana na akulipe mema kwa haya uliyonitendea leo. 20 – Na sasa, angalia, najua ya kuwa hakika utakuwa mfalme, na ufalme wa Israeli utafanyika imara mkononi mwako.

Acha kupigana na kiongozi /mkuu wako kwasababu ya nafasi hautashinda..haijalishi anafanya vibaya kwako kiasi gani..Nyenyekea, tii chini ya mamlaka yake kwa majira hayo. Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kumtoa mtu kwenye kiti ambaye aliwekwa na Mungu, ni Mungu mwenyewe ataamua kulingana na kusudi na majira husika. Wakati wako ukifika hautahitaji kuvuja jasho Mungu atayadhihirsha majira yako mbele za maadui zako nawe utamiliki bila jasho. HII NDIYO NGUVU YA MAJIRA…..

Itaendelea………..

 IMG-20160421-WA0022

FRED MSUNGU

PURE MISSION | +255653318117

(C) 2016

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
The Sow band
Previous post

DOWNLOAD AUDIO: THE SOW BAND - UNYENYEKEVU

Gelax Wa Kristo
Next post

MFAHAMU GELAX WA KRISTO, MWANA HIPHOP INJILI NA MJASIRIAMALI MWENYE NDOTO ZA KIMAPINDUZI YA FIKRA.