SOMO LA FRED MSUNGU: MAJIRA, KUSUDI NA UKOMO WAKE SEHEMU YA PILI. - Gospo Media
Connect with us

SOMO LA FRED MSUNGU: MAJIRA, KUSUDI NA UKOMO WAKE SEHEMU YA PILI.

Mafundisho

SOMO LA FRED MSUNGU: MAJIRA, KUSUDI NA UKOMO WAKE SEHEMU YA PILI.

Katika sehemu ya kwanza wiki iliopita tulijifunza mambo kadhaa juu ya majira hasa kwa kuangalia majira ni nini, kusudi lake kwa ufupi pamoja na sifa /kanuni kuu ya majira

Mambo haya mawili yalitupeleka mpaka kiini kikuu cha funzo ilikua ni sifa kuu ya majira kwamba ni JAMBO LISILO LA KUDUMU. Sasa kama majira ni jambo lisilokua la kudumu maana yake kuna kazi/jambo fulani ambayo ni lazima ifanyike katika majira hayo ili ukomo wake utakapofika matunda ya majira yale au kusudi la majira yale lidhihirike kwa njia ya matokeo, matunda ya wewe kupita katika kipindi husika. Kama jinsi vile ilivyo katika misimu au msimu wa kupanda hua ni wa kupanda, ukichelewa wakati wenzio wanapanda mazao wewe ukaendelea na mambo mengine ujue basi majira yale yakikupita utatakiwa kusubiri tena mpaka majira kama yale yajirudie, na ujue dhahiri kwa kuyakosa majira ya kupanda basi utarajie kukosa mavuno pia, na hata kama utataka kulazimisha kupanda wakati ambao sio wake (kwa kuchelewa) basi ujue kwamba utatakiwa kulipa gharama kubwa sana ili upate kitu bora. wakati ungepanda wakati muafaka wala usingekua na sababu ya kutoa gharama za ziada kwaajili ya shughuli hiyo. Sasa mfano huu pia uko dhahiri sana katika maisha yetu kwamba pale tu utakapokosea na kupishana na majira sahihi ya kufanya jambo ujue kwa hakika kuna matunda utayakosa, na hata kama utataka kufanya kwa wakati wako ujue utatakiwa kulipa gharama ya muda , rasilimali na hata maumivu pia kwasababu tu ya kutofanya jambo kwa muda sahihi, Ninachofundisha hapa ni kwamba jambo muhimu sana kujali sana muda na kufanya jambo sahihi kwa majira sahihi vinginevyo itakugharimu sana, na wakati mwingine unaweza usifanikiwe kabisa.

Kama mwalimu na muandishi ninajua shauku kubwa ya wasomaji ni kutaka kujua je kwa namna gani mtu anaweza akalitambua kusudi pamoja na majira sahihi ya utendeaji kazi wa lile kusudi..? Hili ni swali muhimu sana kwasababu ndilo litakalo leta mzizi wa kuchimba kwa kina ili kupata upana juu ya majira /kusudi pamoja na ukomo wake.

 

                     NJIA KUU MBILI ZA NAMNA YA KUTAMBUA MAJIRA NA KUSUDI

1:KUJUA CHANZO CHA MAJIRA NA KUSUDI

Kabla ya kujua majira liko jambo muhimu sana la kulijua ambalo kwako litakusaidia kuyajua majira na nini cha kufanya , Jambo hilo ni KUSUDI. Bila kujua kusudi hakuna haja ya kuyajua majira kwasababu kabla ya majira lilianza kwanza kusudi na hata kabla yako wewe( majira ya kuzaliwa kwako kudhihirika )

Kusudi ndilo jambo la kwanza kuwapo. Lakini zaidi ya haya yote lipo jambo kuu zaidi ambalo kwako litaleta majibu ya maswali yote…jambo hilo ni kumjua mwenye kusudi na majira ambae ni MUNGU muumbaji wetu…bila huyu huwezi kujua majira wala kusudi maana yeye ndie chanzo cha yote haya.

YEREMIA 1:5

5 – Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Mungu ndie mwenye taarifa sahihi juu ya ujio wako na kwanini ulikuja, kwasababu yeye ndie mfinyazi wetu. (mfinyanzi kabla ya kutengeneza chombo lazima ajue uhitaji wa chombo husika na si uhitaji tu ila kitahitajika wakati gani na katika mazingira gani ! Baada ya kupata majibu yote haya sasa ndipo huja na kifaa maalum kwaajili ya kazi maalum na kwa matumizi maalum. Sasa Mungu ni zaidi ya hawa wote yeye pia hufanya jambo kwa makusudi tena makusudi makuu kuliko ya wanadamu.

Ukisoma hilo andiko la YEREMIA 1 kuanzia mstari wa pili (2) ni baada ya majira ya Yeremia kutimia kwaajili ya kuanza safari ya kulitimiza kusudi Mungu (mwenye ramani ya kusudi na majira) kabla ya kumtuma kazini anamtambulisha kwanza Yeremia kusudi la kuwepo kwake majira yale….kitu kikubwa cha kujifunza hapa ni kwamba Yeremia asingekua na mahusiano na Mungu angeeendelea kuishi ki vyovyote tu maana kamwe asingejua nini anachotakiwa kufanya (KUSUDI) na kwa wakati gani (MAJIRA)

Hii inamaana gani…? Inamaana kwamba chanzo sahihi cha taarifa kuhusu kusudi lako na majira yako ni MUNGU, Ukiona bado unahangaika juu ya nini unatakiwa kufanya katika maisha yako basi ujue mahusiano yako na MUNGU bado hayajawa thabiti, maana yeye ndie mwanzo, chanzo na hakuna kilichofanyika bila yeye

YOHANA 1:1-3

1 – Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu.

2 – Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 – Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakuna chochote kilichofanyika.

                                                           MKAZO (Muhimu)

Sasa ukirudi kwenye Andiko letu simamizi (YEREMIA 1:5) anatumia neno linaloonesha wakati uliopo anasema ” Nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” Hapa nehemia kwa maana nyingine anaambiwa kusudi la kuumbwa au kuwepo kwake. Ukisoma mbele zaidi utaona Yeremia anaanza kulalamika kwamba oooh mimi mdogo.! Lakini Mungu anaendelea kusisitiza kwamba Nehemia alizaliwa kwa kusudi yaani yeye aliletwa kwaajili ya kazi maalum kwa MAJIRA maalum , Sasa yale majira yameshawadia ya Yeremia kutimiza kazi iliyomleta duniani, Jambo lingine la kujifunza hapa kumbe kila jambo hua lina muda wake maalum wa utendaji, kwa hiyo ni vizuri sana kujifungamanisha na huyu mwenye majira ili yeye wakati ukifika akupe ishara ya kuanza.

Kwa hiyo haijalishi umri, kipato au sababu nyingine yeyote majira yako ya kutumiwa kwa kusudi yakifika ni lazima uinuke ufanye ili kutimiza matakwa au kuleta majibu ya maswali katika majira yale husika.

Ni hivi haijalishi kwa namna gani ulizaliwa au mazingira gani umetokea au hali yeyote ulionayo….wewe hata kabla ya kuumbwa kwako Mungu alikupanga na kukuandalia kazi maalum (KUSUDI) ya kuja kufanya katika wakati fulani maalum (MAJIRA)  na hii ndio sababu ukiona mahali fulani lipo jambo tata fulani lisilo na ufumbuzi basi jua kuna mtu fulani mahali fulani kapishana na kusudi lake na majira, Kusudi huambatana na majira kwaajili ya kutimiliza jambo fulani maalumu katika majira husika. Matatizo yote hasara zote ninajipa uhakika kwamba ni matokeo ya mtu mmoja kutokujua nini anachotakiwa kufanya kwa wakati huo. Hivi umewahi kujiuliza leo dunia ingekuaje bila mtu kama Charles Babbage kugundua teknolojia hii ya kutumia vinakilishi (Computer) jibu lake ni rahisi sana pengine hata wewe usingepata fursa ya kusoma nakala hii kwa majira haya. Ninaamini sana hata huu ugunduzi wa vifaa vya kiteknlojia ulioendelea ni kutokana na mwanzo ule wa ugunduzi wa mtu mmoja na si hilo tu mambo mengi sana yangekwama kwasababu ya ukosefu wa hiki kitu kimoja tu ambacho ni mtu mmoja tu ambae amekifanya kiwe na kimekua na manufaa makubwa kwa ulimwengu mzima, Sasa hiyo ndio nguvu na matokeo ya mtu kulitumikia kusudi lake.

Lengo langu hapa nikukuamsha wewe uliyekaa na mawazo makubwa kichwani (maono) lakini unasubiri kesho kuyatekeleza na usijue kwamba majira hayakusubiri na kwa kuchelewa kwako dunia inakua ngumu kwasababu wewe hujataka kulitii kusudi kwa majira sahihi, Hebu amka nakutuma kwa jina la Yesu anza sasa kuliweka hilo jambo katika matendo ili dunia inufaike na uwepo wako kwa majira haya…. Itaendelea…

MINISTRER :FRED MSUNGU

Vilivyopo sokoni kwa sasa
Ni KUSUDI la majira yako (kitabu cha kawaida)
KUSUDI la majira yako ( Audio book)
Hofu ya yasiyojulikana kwa viongozi (Audio CD)
Taarifa ya dharura kwa Africa (DVD)

Dar es salaam vinapatikana duka la vitabu la Savey
Arusha vinapatikana duka la la vitabu kimahama

Kwa walio mikoani wanaweza kutumia namba hizi kwa maswali zaidi +255653318117
fredymsungu@gmail.com

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

More in Mafundisho

To Top