Mafundisho

SOMO LA FRED MSUNGU: MAJIRA / KUSUDI NA UKOMO WAKE SEHEMU YA KWANZA.

Msomaji wangu nimeona ni vyema niuwasilishe ujumbe huu kwako ikiwa ni siku ya kwanza kabisa kuanza mfululizo wa masomo hasa kulingana na hali halisi tuliyonayo tunayoipitia katika taifa letu(Majira husika) Ili kwa pamoja tujifunze namna ya kuyatambua majira na kanuni zake ili yale makosa yaliyojitokeza awali ambayo mpaka sasa tunayaishi matokeo yake yasijitokeze tena kwaajili ya ustawi wa mtu binafsi, taifa pamoja na Ufalme wa Mungu.

Unapoona au kusikia habari za watu waliowahi kua na mafanikio, pesa au fursa fulani na hawanayo tena na wanajutia kutokana na kwamba hakuna matokeo chanya walioyapata au faida kutokana na nafasi ile, Basi ujue lipo tatizo kubwa sababishi ambalo ni KUTOTAMBUA MAJIRA NA MATUMIZI YAKE.

Mtu aliyewahi kumiliki nafasi kubwa na akapotea bila ile nafasi kumnufaisha, Mtu aliewahi kumiliki pesa nyingi na ikafika wakati akafilisika kabisa …ni dhahiri watu hawa pamoja na mambo yote yaliyosababibisha wawe hivyo walivyo kubwa kati ya hayo ni kutoielewa kanuni kuu ya Majira, Lakini kabla ya kuiangalia kanuni ya majira hebu tuangalie kwanza majira ni nini..?

                                                                      MAJIRA NI NINI…?

Majira ni mgawanyo wa muda ambao hudumu kwa kitambo fulani. . . Mfano wa majira ni majira ya kiangazi na majira ya masika; Majira haya ukiyaambatanisha kwa pamoja hufanya muda kusogea mbele na kujikamilisha …..yaani siku ya 1….2…3. hatimaye wiki…hatimaye mwezi, miezi inazaa mwaka. Sasa ndani ya mzunguko huu ndipo upo mgawanyo kwa kitu kinaitwa majira ambayo haya majira sasa hua yapo kwa muda fulani ambao muda huo ukipita basi vipaumbele, utendaji na matokeo hubadilika pia

ANDIKO KUU SIMAMIZI

                                                                         MUHUBIRI 3:

Muhubiri 3 : 1 – Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

(Kwa kila jambo na majira yake) Kila kitu kimetengewa muda wake maalum…HII INAWEZA KUWA TAFSIRI NZURI NA RAHISI ZAIDI HAPO

2 – Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;

3 – Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

4 – Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

5 – Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;

6 – Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;

7 – Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

8 – Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.

9 – Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?

Muhubiri anatuonesha majira mbali mbali na matumizi yake, na jambo kuu ambalo nataka tujifunze pamoja kutoka kwenye hiyo mistari ambayo ni mingi kidogo ni kwamba hakuna tendo lililojirudia kwenye majira yasiyo husika. Yaani kila jambo majira yake yalipopotea nalo linapotea punde, Na kitu pekee kitakachobaki hapo baada ya majira kuisha ni MATOKEO ya utendaji ndani ya majira husika .

Sasa hapa ndipo hua tunajua kwamba jee?…ulitumia majira kwa namna isiyo sawa au namna iliyo sawa kwa kuangalia MATOKEO.

Muhimu kujua kwamba majira huwa hayapigi kelele sana (huwa hayawi maarufu) lakini matokeo hua ni maarufu na yanajionesha dhahiri yawe mazuri au mabaya.

KANUNI / SIFA  KUU YA MAJIRA

Katika andiko lile tulilosoma pale juu utaona muhubiri anatambulisha majira mbali mbali na matumizi yake ambayo ndani yake tunapata kanuni au sifa kuu ya majira kwamba ni KITU KISICHO CHA KUDUMU, Ni muhimu sana ulishike vizuri hili kwamba hakuna hali /majira ya kudumu haijalishi ni mabaya au mazuri kiasi gani jambo la muhimu kujua majira hayawezi kudumu milele.

Sasa kwa kutokulitambua hili wengi tumefeli na kua hivi tulivyo leo kwasababu hatukuyatumia majira ipasavyo hasa kwasababu ya kutokuzingatia kanuni hii kwamba majira hayadumu hua ni ya kitambo tu..! (wakati wewe unasubiri kesho ili ufanye jambo ni vema ujue majira hayatakusubiri kamwe)

Cheo ulicho nacho, kazi ulionayo nafasi ulionayo, shule unayosoma, Hivyo vyote vimekuja kwako kwa majira fulani ambayo muda wake ukiisha hivyo vitu vitapita na kua historia, Sasa ulifanya nini wakati upo kwenye nafasi uliopo kitajulikana baada ya wakati au majira kupita na huu sasa ndio huwa unaitwa wakati wa mavuno.

Itaendelea wiki ijayo..!(fuatilia sehemu ya pili)

Somo limetolewa na FRED MSUNGU, +255653318117

Email: fredmsungu@gmail.com

Facebook: Fred Msungu Page: Pure Mission-Tz

Youtube: FredMsungu/Puretv

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
ANGEL BENARD
Previous post

MUSIC VIDEO: ANGEL BENARD - SALAMA

edna kuja
Next post

YAFAHAMU MAMBO HAYA MATANO YA NGUVU KUHUSU MWIMBAJI EDNA KUJA.