Audio

Audio: Sobre – Piki Piki

Kutoka nchini Zambia leo nimekusogezea wimbo wa mahadhi ya African-Dancehall uitwao Piki Piki kutoka kwa mwimbaji Sobre. Muziki huu umetayarishwa na mikono ya prodyuza TAZ kutoka nchini zambia.

“Piki piki” ni neno lenye asili ya lugha ya nyanja likimanisha “Kuchukua”, Huu ni wimbo wa sifa unaomtukuza Mungu kwa upendo na uwezo wake katika maisha yetu, katika wimbo huu mwimbaji Sobre anaeleza anavyo mshukuru Mungu kwa kumtoa mahali ambapo alikuwa anadharauliwa, kutengwa na kuonekana hafai na sasa amemuweka mahali ambapo anapata heshima na kuthaminiwa katika jamii, huyu ni Mungu ambaye amemfanya aendelee kuimba na kusifa jina lake kila siku.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina imani kuwa utaufurahia na kukubariki, Amen.

 

Download Audio

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Gospel Kid Feat. David Cosmas - Shukurani

Next post

Fahamu mambo 5 unayotakiwa kufanya kila siku ili ufanikiwe