Connect with us

Video: Size 8 Reborn – Holy Holy

Muziki

Video: Size 8 Reborn – Holy Holy

Baada ya kufanya vizuri mwezi Julai kupitia video ya wimbo wake wa kuabudu uitwao Arise mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Kenya Size 8 Reborn kwa mara nyingine tena ameachia tena video yake mpya iitwayo Holy Holy.

Video hii imeongozwa na TrueD Pictures na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Fulforce Music chini ya mikono ya prodyuza Bern Mziki.

“Kwa utukufu wa Mungu Baba yetu tunamwimbia kwa sababu yeye ni Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye ukamilifu katika njia zake zote, Tenga muda kidogo kwa kuacha kuwaza mambo yako mwenyewe bali kusimama katika hofu ya Mungu kwa maana Yeye ndiye.” – alisema  Size 8

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika itakubariki na kukuinua kila siku, Bwana Yesu asifiwe!

Social Media
Facebook: Size 8 Reborn
Instagram: @size8reborn
Twittter: @size8reborn
Youtube: Size8Reborn

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top