Connect with us

Audio: Simoni Feat. Paul Payne – It Ain’t Over

Muziki

Audio: Simoni Feat. Paul Payne – It Ain’t Over

Kutoka nchini Zambia leo nimekusogezea wimbo mpya uitwao “It Ain’t Over” kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini humo akifahamika kwa jina la Simoni hapa akiwa amemshirikisha Paul Payne, Muziki umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Ojo akishirikiana na Geo kutoka studio za Nativez.

It Ain’t Over ni wimbo uliobeba kusudi la kumtia moyo mtu yule aliyekata tamaa akisisitizwa kumtegemea Mungu zaidi hasa pale anapopita kwenye magumu kwa kuwa upendo wa Mungu bado upo juu yake.

Simoni ni mwimbaji wa nyimbo za Injili aliyezaliwa nchini Zambia. Ndoto yake ni kushirikisha watu upendo wa Kristo kupitia nyimbo zake. Anataka kutumia sauti yake kwa kusudi moja na kusudi moja la kuhubiri Injili – Kuwapa matumaini kwa wasio na matumaini na kusambaza neema ya Neno la Mungu na upendo wake kwa wanadamu. Alizaliwa na kukulia katika familia ya Kikristo, wazazi wote ni walimu na wachungaji. Yeye ni mtoto wa tatu aliyezaliwa katika familia ya watoto wanne (4).

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakuwa wimbo huu ambao nina imani kuwa utakubariki na kukuinua, Amen.

 

Download Audio

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top