Habari

Kongamano la Kuambukizwa Neema ya Kinabii Kuanza Juni 1

Nabii Clear Malisa wa kanisa la Kingdom Embassy liliopo Ubungo River side Jijini Dar es salaam anakukaribisha kwenye ibada ya siku mbili ya Ushauri na kuambukizwa neema ya kinabii (Mentorship Program and Impartation) itakayofanyika Juni ya tarehe 1 na 2, katika Ukumbi wa Hotel ya Kebby’s uliopo Bamaga-Mwenge kuanzia saa kumi jioni.

Akiongea na mwandishi wa habari wa gospomedia.com Nabii Clear Malisa amesema kuwa kongamano hilo litakuwa limebeba ibada yenye nguvu na ujazo wa aina yake wa Roho Mtakatifu katika kuanza mwezi mpya katika mwaka 2018, Hivyo watu wote wamesisitizwa kufika bila kukosa ili kuweza kupokea Baraka na Neema za Mungu kupitia huduma ya mtumishi wake Nabii Clear Malisa.

Kwa mawasiliano zaidi juu kongamano hili, kujisajili na jinsi kufika wasiliana na Nabii Clear Malisa kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 787 749 719
Facebook: Prophet Clear Malisa
Instagram: @prophetclearmalisa YouTube: Prophet Clear Malisa

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Davis Kiarie Feat. Kes Mbogoh - Yesu Pekee

Next post

Video | Audio: Abeid Makarabo - Afya ya Roho