Connect with us

Sikiliza & Download Music Audio: Sarah Ndosi Feat Bomby Jonson-Pumzi Yako

Muziki

Sikiliza & Download Music Audio: Sarah Ndosi Feat Bomby Jonson-Pumzi Yako

Kutoka Dar es salaam Tanzania, gospomedia.com leo tunakualika uweze kusikiliza na kupakua wimbo mpya uitwao Pumzi Yako kutoka kwa muimbaji mahiri wa muziki wa live anayefahamika kwa jina la Sara Ndosi akiwa amemshirikisha muimbaji mahiri Bomby Johnson ukiwa umetengenezwa ndani ya studio ya Push Up Records chini ya mikono ya producer Innocent Mujwahuki akishirikiana na producer Emmanuel Gripa kutoka jijini Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia.com muimbaji Sarah Ndosi amesema kuwa wimbo huu wa Pumzi Yako ni moja kati ya nyimbo zinazopatikana kwenye album yake mpya yenye mkusanyiko wa nyimbo saba iliyo kwenye mfumo wa Audio CD inayokwenda kwa jina la Natamani ambayo ina mkusanyiko wa nyimbo zenye nguvu ya baraka na zenye kuinua sana.

Kitu kikubwa na tofauti kilicho katika mkusanyiko wa album hii mpya ni kwamba nyimbo zote zimetengenezwa kwenye mahadhi tofauti tofauti kama vile Afro Jazz, Rock, Traditional, Slow Worship na Sebene ili usiweze kuchoka kuisikiliza album hii mara kwa mara licha ya utofauti huo mkubwa album hii pia imeandaliwa kwa kiwango cha kipekee sana ikiwa na karatasi maalumu ya mashairi ya nyimbo zote zilizo katika album hii ili kumsaidia msikilizaji aweze kuyashika mashairi ya nyimbo hizo kwa urahisi zaidi.

Kwa yeyote anayehitaji nakala ya album hii mpya iitwayo Natamani kutoka kwa muimbaji Sara Ndosi unaweza kutembelea vituo vifuatavyo studio ya Faith Music Lab iliyopo Kinodoni biafra, Kanisa la VCCT Mbezi kawe na Duka la vitabu Packway Bookshop Bamaga.

gospomedia.com tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu uweze kuusikiliza na kuupakua wimbo huu kisha washirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kuisambaza Injili kwa watu wengi zaidi ili wapate kubarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu wa Pumzi Yako na hakika utabarikiwa sana. Karibu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kupata nakala ya album hii au huduma ya mialiko kutoka kwa muimbaji Sarah Ndosi wasiliana naye kupitia.
Simu/WhatsApp: +255 656 521 114
Facebook: Sarah Shilla-Ndosi
Instagram: @sarandosi
Youtube: NAS Ndosi
Email: sarah.shilla@yahoo.com
Website: www.sashi.co.tz⁠⁠⁠⁠

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA instagram: @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top