Connect with us

Sikiliza & Download Music Audio: Fadhili Kibanti-Wakati wa Bwana

Muziki

Sikiliza & Download Music Audio: Fadhili Kibanti-Wakati wa Bwana

Kutoka Dar es salaam Tanzania, gospomedia.com leo inamtambulisha kwako muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Fadhili Kibanti ambaye siku ya leo anautambulisha wimbo wake mpya unaoitwa Wakati wa Bwana ukiwa umetengenezwa ndani ya studio ya Mega hit kutoka jijini Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia.com muimbaji Fadhili Kibanti amesema kuwa wimbo huu wa Wakati wa Bwana ni moja kati ya nyimbo 8 zinazokamilisha album yake ya kwanza iliyo kwenye mfumo wa Audio Cd inayokwenda kwa jina la Hakuna Linaloshindikana Kwa Mungu ambayo mpaka sasa ipo tayari ila bado haijaingia sokoni kwakuwa bado anatafuta msambazaji na mdhamini atakayemsaidia kuinyanyua album yake na huduma yake kwa ujumla.

gospomedia.com tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu uweze kuusikiliza na kuupakua wimbo huu kisha washirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kuisambaza Injili kwa watu wengi zaidi ili wapate kubarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu wa Wakati wa Bwana na hakika utabarikiwa sana. Karibu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko na mwimbaji Fadhili Kibanti wasiliana naye kupitia.
Simu/WhatsApp: +255 656 867 582
Facebook: Fadhili Kibanti
Instagram: @fadhilikibanti
Twitter: @fadhilikibanti

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA instagram: @gospomedia

TRENDING

To Top