Connect with us

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Stephen Wandera-Hapa Duniani

Audio

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Stephen Wandera-Hapa Duniani

Kutoka nchini kenya anaitwa Stephen Wandera mwimbaji wa nyimbo za Injili na huu ni wimbo wake mpya unaoitwa Hapa Duniani ikiwa ni moja ya wimbo unaopatikana kwenye album yake iitwayo Mushibhala Muno akiongea na gospomedia.com muimbaji stephen wandera amesema kuwa lengo la wimbo huu ni kuwahimiza watu wasitume mamlaka yao vibaya hapa duniani na kuwasihi kumtumikia Mungu katika roho na kweli.

Stephen Wandera ni muimbaji ambaye alianza kuimba muziki akiwa mdogo na alitambua kipawa chake akiwa anahudumu kanisani na mpaka kufikia mwaka wa 2007 aliweza kuwa na uwezo wa kutunga nyimbo na kuimba na mpaka kufikia sasa anamshukuru Mungu kwakuweza kufanya album tatu ambayo ya kwanza ni YESU NDIYE JIBU, ya pili ni Wanadamu Jamani na ya tatu inaitwa Mushibala Muno ambayo imebeba wimbo wa Nitengeneze ambao pia unapatikana hapa gospomedia.com.

gospomedia.com tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu uweze kusikiliza na kuupakua wimbo huu kisha uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kuisambaza Injili kwa watu wengi zaidi ili wapate kubarikiwa na kuinuliwa kiroho kupitia wimbo huu wa Hapa Duniani kutoka kwa muimbaji stephen wandera na hakika utabarikiwa sana. Karibu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji stephen wandera kupitia
Simu/WhatsApp: +254 711 353 966
Facebook: Stephen Wandera Namudiru
Instagram: @stephenwandera E-mail: namudirus@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Audio

To Top