Audio

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Stanley Qamara – Kilicho Bora

Kutoka jijini Arusha Tanzania gospomedia.com leo inamtambulisha kwako mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Stanley Qamara wimbo huu unaitwa Kilicho Bora ukiwa ni wimbo ulioandaliwa na kutengenezwa ndani ya studio za Habari Maalum chini ya usimamizi wa kampuni ya Genecic iliyopo jijini Arusha.

Akiongea na timu ya gospomedia.com stanley qamara yeye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili na mzaliwa wa Arusha ambapo mpaka sasa anaishi huko. Alianza kuimba muziki akiwa shule ya Jumapili(Sunday School) akiwa mtoto baadae aliacha kabisa kuimba mpaka alipofika chuo kikuu cha Dodoma mwaka 2013 alijiunga na Christian fellowship praise team (C.F) chuoni hapo.

Muimbaji Stanley Qamara pia aliimba na Campus Night Dodoma mass choir kisha kujiunga na darasa la awali la muziki chini ya mkufunzi Aron Urio kitengo cha muziki UDOM. Wakati huo akajiunga na kundi lililoitwa Sparks Of Christ. Baada ya kumaliza masomo yake alirudi tena Arusha na kuendelea kufanya muziki wa Injili na sasa ameanza kufanya project zake binafsi chini ya usimamizi wa kampuni ya Genecic na huu ni wimbo wake wa kwanza unaokwenda kwa jina la Kilicho Bora ulioandaliwa katika studio za Habari Maalum chini ya usimamizi wa kampuni ya Genecic.

gospomedia.com tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu kusikiliza na kupakua wimbo huu wa Kilicho Bora kutoka kwa mumbaji Stanley Qamara na usiache kumpa sapoti kwa kuwashirikisha wengine wimbo huu kwa kadri uwezavyo ili Injili iweze kuwafikia wengi zaidi duniani kote na hakika utabarikiwa sanaKaribu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Stanley Qamara kupitia
Simu/WhatsApp: +255 656 450 681
Facebook Page: Genecic
Instagram: @genecicpromotions
Youtube: Genecic promotions

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Henry Sanga Feat Christina Shusho - Nipeni Muda

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Music: Lydia Charles - Twakuabudu