Connect with us

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Novic BCvm Feat Dolaa – Okoka Sasa

Muziki

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Novic BCvm Feat Dolaa – Okoka Sasa

Kutoka jijini Arusha Tanzania, leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuletea wimbo mpya uitwao Okoka Sasa kutoka kwa muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop anayefahamika kwa jina la Novic BCvm safari hii akiwa amemshirkisha Dolaa wimbo ukiwa umetengezwa na producer anayefahamika kwa jina la DJ.DNA.

gospomedia.com tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu kusikiliza na kupakua wimbo huu uitwao Okoka Sasa kutoka kwa muimbaji Novic BCvm akiwa amemshirikisha Dolaa.

Unaweza kumpa sapoti yako kwa kuwashirikisha watu wengine zaidi wimbo huu kwa kadri uwezavyo ili Injili iweze kuwafikia watu wengi na kuwakoa na hakika utabarikiwa sanaKaribu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi na huduma za mialiko wasiliana na mwimbaji Novic BCvm kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 717 076 016
Facebook: Novic BCvm
Instagram: @novicbcvm
Twitter: De Ferrary
Soundcloud: Novic BCvm
Email: wanurutz@gmail.com

Na haya ni mashairi yanayopatikana kwenye wimbo huu:

OKOKA SASA LYRICS

Intro: Novic BCvm

Wa NURU……. Dolaa………. Novic….BCvm

Okoka……………sasa

Okoka…………….sasa

Okoka…………….sasa

Okoka, okoka

Chorus: Novic BCvm

Buda Yesu anakupenda…..Okoka sasa

Dada nawe tambua anakupenda…..Okoka sasa

Muda ndo huu ungali unahema….Okoka sasa

Mkumbuke Muumba ungali ni kijana……..Okoka sasa

Verse 1: Novic BCvm

Yesu anakuita njoo, kuokoka usione soo

Uiponye yako roho, na Jehanum ya moto

Tusingekuwa tunahitaji msaada wala Bwana Yesu asingekuja

Asingeaibika wala kuchomwa ubavuni damu isingevuja

Alinija mimi na wewe tuwekwe huru, tukombolewe

Tupewe nuru tuangaziwe nguvu za giza tuzitawale

Ametufutia hatia ya ujinga wote tul’opitia

Kweli na neema katuletea haki ya bure tunapokea

Kwanini ndugu umkatae, neema ya bure ipokee

Kanitumia hata nnaye-rap jinsi ulivyo Injili ikufikie

INJILI sio huu wimbo, INJILI sio mtindo

Ni Uweza wa Mungu uletao Wokovu amini uone jinsi ulivyo

Kakuumba yeye na hivyo, anakupenda jinsi ulivyo

Anataka akuboreshe ili uishi vile atakavyo

Kuokoka ndugu ni buree! Maamuzi unayo wewe

Ili kuingia mbinguni Bwana Yesu ndiye njia pekee

Chorus: Novic BCvm

Buda Yesu anakupenda…..Okoka sasa

Dada nawe tambua anakupenda…..Okoka sasa

Muda ndo huu ungali unahema….Okoka sasa

Mkumbuke Muumba ungali ni kijana……..Okoka sasa

Verse 2: Dolaa

Njia ya mpumbavu imenyooka machoni pake

Njia za upotevu iko sawa mbele zake

Walijua amefufuka bado hawakusadiki

Wanatafuta uongo na kufuata ushabiki

Deni unaloweka leo, peke yako utalipia

Malipizi yakirudi hakuna wa kumlilia

Ukitenda mabaya watu watakusifia

Ukianguka leo wote watakukimbia

Okoka sasa deni aliishalipia, dhambi tulileta

Ila yeye katufia

Utamwona sio tu kumsikia damu yake ya utakaso

Wa maelfu na mamia

Ukiikataa kweli haibadiliki kuwa uongo

Tatizo sio imani ila umempa nani moyo

Jua lina umri mwingi nguvu yake pale pale

Hivyo Mungu kabla ya jua akafanya vitokee

Chorus: Novic BCvm

Buda Yesu anakupenda…..Okoka sasa

Dada nawe tambua anakupenda…..Okoka sasa

Muda ndo huu ungali unahema….Okoka sasa

Mkumbuke Muumba ungali ni kijana……..Okoka sasa x2

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top