Audio

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Borne Kingz – Hello

Kutoka jijini Dar es salaam, Tanzania gospomedia.com leo inautambulisha kwako wimbo mpya kutoka kwa kundi mahiri la waimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili kwa miondoko ya Hiphop linalofahamika kwa jina la Borne Kingz wimbo huu unaitwa Hello ukiwa umetengenezwa ndani ya studio za Pushup records chini ya mikono ya producer Innocent Mujwahuki kutoka mjini Dar es salaam.

Borne kingz ni kundi linalounganisha vijana watatu ambao ni Ellyjoh, Lamasias pamoja na Elandre. Kundi hili liliundwa tangu mwaka 2011 kwa nia njema ya kutumika kwenye ufalme wa Mungu. Maana halisi au kirefu cha BORNE KINGZ ni “Bearing the Mark of the King” ikimaanisha “Wabeba Chapa ya Kifalme”.
Wakiongea na gospomedia.com HELLO ni nyimbo ilitengenezwa na producer Inocent Mujwahuki ndani ya studio ya Push up Records, ikiwa ni nyimbo yao ya kwanza rasmi (official release) kutoka kwenye album yao ya kwanza itakayobebwa na jina la ”AFTERMATH” ambayo mpaka sasa haijatoka rasmi ikiwa  bado inaendelea kuandaliwa chini ya mikono ya producer Mujwahuki na Neshi kutoka ndani ya studio ya Push-up records.

gospomedia.com inakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu uitwao Hello kutoka kwa kundi la waimbaji nyimbo za Injili linalofahamika kwa jina la Borne Kingz pia usiache kuwashirikisha (kushare) watu wengi zaidi wimbo huu kwa kadri uwezavyo ili Injili iweze kuwafikia watu wengi zaidi mahali pote duniani na hakika utabarikiwa sanaKaribu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na kundi la waimbaji hawa wa kundi la Borne Kingz kupitia:

Simu/Whatapp: +255 717 057 457
Facebook page: Borne Kingz
Instagram: @bornekingz
Email: bornekingztz@gmail.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

OnStage: Rogate Kalengo Alivyoimba Live Kwenye Uzinduzi wa Album Yake Mpya Kuna Namna, Uhuru Morovian Church.

Next post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Mo Shilla feat Thelma - Forgiven