Siku Nane za Shilo, Moto utawaka Disemba 3 - 10, 2017 Kanisa la Mlima wa Moto - Gospo Media
Connect with us

Siku Nane za Shilo, Moto utawaka Disemba 3 – 10, 2017 Kanisa la Mlima wa Moto

Matukio

Siku Nane za Shilo, Moto utawaka Disemba 3 – 10, 2017 Kanisa la Mlima wa Moto

Na Mwandishi Wetu;

Kongamano kubwa la maombi na maombezi kwa taifa linalofahamika kwa jina la SHILO linaloandaliwa na kufanyika kila mwaka chini ya mchungaji kiongozi Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, kwa mara nyingine tena anakukaribisha kwenye kongamano hili kubwa linalotarajiwa kuanza siku ya jumapili ya Disemba 3 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka Disemba 10, 2017 ambapo ndipo kilele cha kongamano hilo litakalokuwa linafanyika katika kanisa la Mlima wa Moto lililopo Mikocheni B jijini Dar es salaam.

Kongamano hili limebeba kauli mbiu isemayo ”BWANA KUJIFUNUA TENA KATIKA TAIFA LETU, AFYA ZETU, UCHUMI WETU, NDOA ZETU, MASOMO YETU, UZAO WETU, HUDUMA ZETU, MAISHA YETU, FAHAMU ZETU, MALENGO YETU N.K”

Akizungumza na gospomedia.com Mhe. Bishop Dr.Getrude Rwakatale amesema kuwa mbali ya kumshukuru Mungu kwa kuiweka nchi salama mpaka sasa, lakini pia kongamano hili litatumika kumuombea Raisi wa awamu ya Tano Dr. John Pombe Magufuli na serikali ya awamu ya Tano.

”Tumekuwa Tukiandaa kongamano hili la Shilo kila mwaka kwa ajili ya kufanya maombi na maombezi kwa siku saba kuelekea kuumaliza mwaka lakini kwa mwaka huu tutalitumia kongamano hili kumuombea Raisi Dk. John Pombe Magufuli na viongozi wote wa serikali ya awamu ya Tano kwa muda wa siku nane mfululizo.” Alisema Mchungaji Getrude Rwakatale

Alisema wateule wa Mungu hawana budi kusimama katika nafasi zao kwa niaba ya watanzania wote katika kumshukuru Mungu kwa hali ya amani na utulivu iliyopo nchini, pia kumshukuru Mungu kwa kuwapatia Raisi mzuri mwenye kiu ya kuwapigania watanzania, pia kuzidi kumkabidhi mikononi mwa Mungu ili azidi kumpa hekima na maarifa katika kipindi chote cha uongozi wake.

Aliongeza kuwa kongamano hili litakusanya watu kutoka maeneo mbalimbali bila kujali madhehebu yao, dini zao wala makabila yao lengo likiwa ni kufanya kusanyiko hilo kutumia siku hizo nane katika kumtafakari Mungu na kutoa shukrani zao kwa yale ambayo Mungu amewatendea kwa kipindi cha mwaka mzima.

Kongamano hili hufanyika mara moja kwa mwaka na hii ikiwa ni mara ya tano tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013 na litahusisha maaskofu, wachungaji na watumishi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania akiwemo Bishop Dr. Dustan Maboya kutoka Arusha, Pastor Paul Kuria kutoka jijini Nairobi Kenya na watumishi wengine wengi, lakini pia kutakuwa na waimbaji na kwaya mbalimbali ambazo zitahusika katika kuhudumia watu kwa njia ya muziki wa Injili, kupamba na kusindikiza kongamano hilo.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Matukio

To Top