Connect with us

Sheria mpya za Vatican zatoa adhabu kali kwa wanyanyasaji wa kingono

Sheria mpya za Vatican zatoa adhabu kali kwa wanyanyasaji wa kingono

Habari

Sheria mpya za Vatican zatoa adhabu kali kwa wanyanyasaji wa kingono

Na Mwandishi Wetu,

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis amebadilisha sheria za kanisa hilo na sasa anasema itakuwa uhalifu kutekeleza unyanyasaji wa kijinsia.

Ni mabadiliko makubwa ya sheria ya uhalifu kwa karibia miaka 40 iliopita. Sheria hiyo mpya , inafanya unyanyasaji wa kijinsia , kuwaandaa watoto kwa ngono, kumiliki kanda za video ama picha za ngono za watoto na kuficha unyanyasaji kuwa uhalifu mkubwa chini ya sheria ya Vatican.

Papa alisema kwamba lengo lake moja lilikuwa kupunguza idadi ya visa ambapo adhabu iliiachiwa kutekelezwa na watawala.

Mabadiliko ya sheria hiyo yalichukua takriban miaka 11 kutengeneza na inashirikisha mchango kutoka kwa makanoni au viongozi wa dini wa kanisa hilo na wataalamu wa sheria ya uhalifu .

Kanisa la katoliki limekumbwa `na ripoti za unyanyasaji unaotekelezwa na wahubiri huku baadhi ya viongozi wa dini pia wakihusika katika kuficha unyanyasaji katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Waathiriwa na wakosoaji walilalamika kwa miongo kadhaa kwamba sheria zilizokuwepo, zilipitwa na wakati , zikidaiwa kuficha washukiwa.

Sheria hiyo mpya inabadili mabadiliko ya mwisho yaliofanywa na papa John wa pili 1983. Imebuniwa kuwa na uwazi kwa lugha fulani na inatoa ruhusu kwa maaskofu kuchukua hatua iwapo kutakuwa na malalamishi.

Sheria hiyo itaanza kutumika tarehe 8 mwezi Disemba , Pia inakataa kutawaza wanawake , kurekodi wanaokiri na kufanya udanganyifu.
Je ni mabadiliko gani?

Sheria hiyo ya Vatican pia inatambua kwamba watu wazima pamoja na watoto wanaweza kuathiriwa na wahubiri ambao hutumia vibaya mamlaka yao.

Awali kanisa hilo liliamini kwamba watu wazima wanaweza kuruhusu ama kukataa kutokana na umri wao na halikutilia maanani kwamba watu wazima pia wanaweza kuwa waathiriwa hususan iwapo hakuna usawa wa mamlaka.

Sheria hiyo inasema muhubiri anaweza kupoteza wadhfa wake iwapo alitumia nguvu, kutoa vitisho au kutumia vibaya mamlaka yake kutekeleza vitendo vya unyanyasaji wa kingono.

Kwa mara ya kwanza watu wa vyeo vya chini kwenye mfumo wa kanisa kama vile wasimamizi wanaweza kuadhibiwa kwa unyanyasaji kama vile kupoteza kazi zao , kulipa faini ama kuondolewa katika jamii zao.

Chanzo: BBC

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Advertisement

TRENDING

To Top