Audio

Audio: Shasha Solo – We ni kila kitu kwangu

Kutoka jijini Dar es salaam leo nimekusogezea wimbo mzuri na wenye kubariki uitwao We ni kila kitu kwangu kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahmika kwa jina la Shasha Solo, muziki huu umetayarishwa na mikono ya prodyuza Dady One-touches kutoka ndani ya studio za Shega Records.

Kwa mujibu wa mwimbaji Shasha Solo amesema kuwa kitu ambacho kimemsukuma kuandika wimbo huu ni kutokana nyakati tofauti tofauti za maisha ambazo yeye huwa anapitia na kumfanya ashindwe kusonga mbele lakini pamoja na yote hayo bado anaamini Mungu ana kusudi na yeye licha ya changamoto na majaribu anayopitia kwa nyakati tofauti anaamini ipo siku moja atasimama na kupata nguvu mpya, kwakuwa Yesu kwake ni kila kitu.

Mbali na hayo mwimbaji Shasha Solo amesema kuwa kwasasa anahitaji kupata mtu ambaye ataweza kuiwezesha huduma yake kifedha ili aweze kuwahudumia watu wengi wenye kiu ya neno la Mungu kupitia muziki wenye kiwango bora zaidi huku akiamini ukuu wa Mungu utakwenda kudhihirika kwa lile kusudi ambalo ameweka ndani yake.

Nina Imani kuwa kupitia wimbo huu mzuri utapata nguvu mpya na kubarikiwa kila utakapokuwa unausikiliza, mfanye Yesu awe kila kitu kwako naye atatenda miujiza mikubwa katika maisha yako, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Shasha Solo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 716 757 407
Facebook: Shasha Solo
Instagram: @shasha_solo
Youtube: shasha solo

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Suzie P. Mahalu - Mungu Akikubariki | Nikuite jina gani

Next post

Audio: Neema Ng'asha - Naamini