Connect with us

Shadrack Robert kuachia video yake mpya siku ya Pasaka

Habari

Shadrack Robert kuachia video yake mpya siku ya Pasaka

Moja kati ya waimbaji wanaofanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania hutaacha kumzungumzia mwimbaji Shadrack Robert akiwa kati ya waimbaji ambao wanaonyesha jitihada za kuitangaza Injili kupitia muziki na sasa akiwa anapiga hatua kimataifa baada ya kuweka wazi ujio wake mpya wa video ambayo anatarajia kuiachia siku ya pasaka.

Akizungumza na gospomedia.com mwimbaji Shadrack Robert amesema kuwa video yake mpya inayobebwa kwa jina la Siyabonga Jesu inatarajiwa kuachiwa tarehe 1 April 2018 ikiwa ni siku ya Pasaka.

”Siyabonga Jesu ni neno la lugha ya Kizulu inayozungumzwa nchini ikiwa na maana ya Asante Yesu ikiwa ni wimbo wa kumrudishia Bwana Yesu Sifa na utukufu kwa maana kwa upendo wake sisi tumepata wokovu na utakaso, kila mmoja kwa nafasi yake amsifu Bwana kwa nyimbo za sifa na utukufu, kwa maana kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” – Alisema Shadrack

video hii imefanyika nchini afrika kusini ikiwa imeongozwa na Director Decha, na yawezekana hii ikawa ni hatua moja kubwa ambayo inaweza kuleta matokea mazuri na makubwa katika kazi zake na huduma yake kwa ujumla.

Kupitia chaneli yako pendwa ya Gospo TV tutakusogezea video hii ambayo tunaamini itakubariki na kuifurahia huku ukimtukuza Bwana Yesu kwa yale ambayo amekutendea katika maisha yako, Ameen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Shadrack Robert kupitia
Simu/WhatsApp: +255 767 897 260
Facebook: Shadrack Robert
Instagram: @shadrackrobert
YouTube: Shadrack Robert
Email: thisisshadrack@gmail.com

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Habari

To Top