Connect with us

Selena Gomez kwa machozi aweka wazi ushuhuda wake na kusema ‘Mimi ni Mtoto wa Mungu’

Habari

Selena Gomez kwa machozi aweka wazi ushuhuda wake na kusema ‘Mimi ni Mtoto wa Mungu’

Na Mwandishi Wetu;

Muigizaji wa filamu na staa wa muziki wa pop Selena Gomez amefunguka juu ya ushuhuda wa maisha yake na uamuzi wake wa kurudi kwa Mungu katika Mkutano wa Hillsong mwaka huu huko Los Angeles.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishiriki ushuhuda wake kwa njia ya barua, ambayo inaelezea maisha yake toka alivyokuwa mtoto hadi sasa.

Gomez alikiri maisha yake ya Hollywood yalikuwa ni ya kuchanganya na yenye uchungu mwingi, mpaka alipogundua ni kwa kiasi gani Mungu anampenda.

“Miaka minane baadaye, utakuwa umeketi katika huduma na kila kitu ndani yako kitasimama. Mungu ambaye amekuwa akikutafuta kila wakati atakuwa na hisia inayoonekana, Roho Mtakatifu atasema kwa sauti zaidi kuliko kitu chochote kilichokutafuta.”

Gomez alisema imani yake na umaarufu wake umekuwa kwa kiasi kikubwa toka alipokutana na Yesu wa kweli miaka miwili iliyopita.

Ushuhuda wa Gomez umetangaza kwa ujasiri imani yake katika kristo

“Selena, wewe watosha! Si kwa sababu umejaribu kwa bidii, sio kwa sababu umependa kwa bidii au kuweka uso wako bora, sio kwa sababu umepewa jukwaa kubwa na si kwa sababu wengine wanakuambia watosha,'” alisema. “Wewe watosha kwa sababu wewe ni mtoto wa Mungu ambaye alikuwa akikufuatilia tangu mwanzo .. Wewe watosha kwa sababu neema yake imekuokoa na kukufunika.”

Itazame video ya ushuhuda wake hapa chini.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Habari

To Top