Video | Audio: Sayuni Mrita - Nitashinda Tu - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Sayuni Mrita – Nitashinda Tu

Video | Audio: Sayuni Mrita – Nitashinda Tu

Baada ya kimya cha kitambo kidogo kwa mara nyingine tena mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kama Sayuni Mrita kutoka mjini Morogoro ameachia video ya wimbo wake mpya iitwayo Nitashinda Tu.

Video hii imeongozwa na director Mbagwa, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Ritha’s Records chini ya mikono ya prodyuza Kingson na Papaa Denilson.

“Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kuandaa wimbo huu wa NITASHINDA TU ukiwa ni wimbo uliobeba ujumbe wa Roho Mtakatifu kwa watu wote, Ni wimbo Unaomtia mtu moyo aweze kusimama katika neno la Mungu hata kama wanakutana na hali ngumu inayoonekana kama usiku kwao. Mungu anatuwazia mema na ametuhakikishia ushindi, Akiwa upande wetu hatutaogopa wala kutikisika, tuna UJASIRI, Mungu akubariki unapousikiliza kila siku.” – alisema Sayuni Mrita.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki na kukuinua kila wakati utapokuwa unatazama na kusikiliza, Amen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma watiliana na mtumishi wa Mungu Sayuni Mrita kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 686 815 115
Facebook: Sayuni Mariki-Mrita
Instagram: @sayuni_mrita
Youtube: Sayuni Mariki-Mrita

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top