Audio: Rungu La Yesu Feat. Pastor Florian Katunzi-Utakatifu Remix - Gospo Media
Connect with us

Audio: Rungu La Yesu Feat. Pastor Florian Katunzi-Utakatifu Remix

Audio

Audio: Rungu La Yesu Feat. Pastor Florian Katunzi-Utakatifu Remix

Kutoka katika kundi maarufu la muziki wa Injili kwa mtindo wa HipHop linalofhamika kwa jina la “Yesu Okoa Mitaa” leo kwa utukufu wa Mungu nimekuletea wimbo uliobeba ujumbe wa pekee uitwao “Utakatifu” kutoka kwa kiongozi wa kundi hilo maarufu kama Rungu la Yesu hapa akiwa amemshirikisha mchungaji kiongozi Florian Katunzi wa kanisa la EAGT City Centre, Hii ikiwa ni marudio ya wimbo aliouachia mwaka 2016 uliobebwa kwa jina la Utakatifu.

Muziki huu umetayarishwa na mikono ya prodyuza Eribless akishirikiana na prodyuza Amyz na kurekodiwa ndani ya studio za Blessed Music Industry (B. M. I.) zilizopo jijini Dar es salaam.

“Utakatifu” ni wimbo uliobeba ujumbe wenye kuwaasa watu wote kuwa ili tuweze kuwa karibu zaidi na Mungu lazima tukubali kuokoka na kuishi maisha ya matakatifu katika kila jambo na kila kitu tunachofanya maana utakatifu ndio kila kitu katika kufungua milango ya baraka, neema na rehema za Mungu katika maisha yetu sisi Binadamu, hivyo kila mmoja kwa wakati wake atafakari ujumbe huu kwa kina juu ya maisha anayoishi sasa je yanamtukuza Mungu? na kama hayamtukuzi Mungu basi yatupasa tutubu dhambi ili tuweze kuwa wapya na kuishi maisha safi yenye kumpendeza Mungu ili Baraka zake zisiwe mbali nasi.

“SHALOM WAPENZI WA MUZIKI WA HIP HOP GOSPEL… KUTOKANA NA UZITO WA UTAKATIFU IMENILAZIMU KURUDIA KUUFANYA WIMBO HUU NA HUYU KUHANI MCHUNGAJI FLORIANI KATUZI WA EAGT CITY CENTER  UTAMSIKIA HUMO  AKIPIGILIA UTAKATIFU KAMA MSUMARI WA MOTO KWA WANAOPENDA DHAMBI NA DINI ZAO… KAMA UTAKATIFU ULIVYO, ILI UFANIKIWE NI LAZIMA UZINGATIE KUISHI KITAKATIFU.” – Rungu la Yesu

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye ujumbe utakaokubadilisha na kukujenga, Barikiwa.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Rungu la Yesu kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 712 348 032
Facebook: Rungu la Yesu
Instagram: @rungulayesu

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top