Habari

Hivi ndivyo Rosebud Children’s Foundation Ilivyozindua kituo cha watoto kujisomea

Jumanne ya tarehe 1.05.2018 taasisi ya isiyo ya kiserikali  inayofahamika kama Rosebud Children’s Foundation ilizindua rasmi kituo cha kujisomea watoto maeneo ya Mji mwema, Kigamboni.

Akizundua Rasmi kituo hicho wakili wa kujitegemea Bi. Beata Fabian ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameipongeza Rosebud kwa kuonyesha nia ya kupambana na adui mkubwa wa Taifa ambaye ni ujinga.

Bi. Beata Fabian akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wenye nidhamu kituoni hapo.

Pia Bi. Beata amewataka wazazi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kuunga mkono juhudi za Rosebud Childrens Foundation katika kuelimisha jamii hususani watoto ili Taifa liwe na watu wanaojitambua.

Kwa upande mwingine akiongea kwa niaba ya Rosebud Children’s Foundation Bi. Upendo Mbaga ametanabaisha kwamba wazo la kuanzisha kituo hicho lilipatikana mwaka 2016 ambapo yeye na wenzake walikuwa na wiwa wa kurudisha fadhila kwa jamii na ndipo hapo mchakato wa kuanzisha Rosebud Children’s Foundation ulipoanza.

Taasisi ya Rosebud Childrens Foundation imetoa wito kwa jamii na wadau wa maendeleo kuiunga mkono taasisi hiyo kwa hali na mali ili iweze kukamilisha azma yake ya kulikomboa Taifa kutoka kwenye ujinga.

Uongozi wa Rosebud Chidrens Foundation wakiwa na mgeni rasmi Bi. Beata Fabian (wapili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja katika siku ya hafla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu Taasisi hii na kuiunga mkono wasiliana na uongozi wake  kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 752 056 168 au +255 754 415 771
Instagram: @rosebudchildrensfoundationtz

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Godwin Maimu atangaza fursa mpya kwa waimbaji wa nyimbo za Injili

Next post

Walter Chilambo Kuachia Asante Album Juni 3, 2018