Connect with us

Audio: Rose O. Mollel Chipe – Hakuna Kama Yesu

Muziki

Audio: Rose O. Mollel Chipe – Hakuna Kama Yesu

Audio: Rose O. Mollel Chipe – Hakuna Kama Yesu

Kutoka jijini Arusha Tanzania leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tunautambulisha kwako wimbo mpya uitwao Hakuna Kama Yesu kutoka kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Rose Mollel (Chipe) wimbo huu umefanyika ndani ya studio za Aflob chini ya mikono ya producer Alex Lobulu kutoka jijini Arusha,  wimbo huu utapatikana kwenye moja ya album zake mpya anazotarajia kuziwekea wakfu na kuachia rasmi album hizo mpya ambayo moja inabeba jina la Hakuna Kama Wewe ikiwa katika mfumo wa DVD na nyingine itakuwa kwenye mfumo wa Audio CD ambapo album zote hizi zitazinduliwa rasmi Tarehe 02.07.2017 katika kanisa la KKKT KIRANYI, Barabara ya silentini, Sakina kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi mpaka saa tatu asubuhi.

Akiongea na timu ya gospomedia.com muimbaji Rose Mollel (Chipe) amesema kuwa uzinduzi huo pia utaambatana na Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu kuanzia saa sita kamili mchana na kusindikizwa na waimbaji mbalimbali kama vile Upendo Nkone, Lembo Junior, Machalii wa Yesu, Shadrack Robert, Baraka Massa, God’s Surrender, Angelina Francis, Upendo Mbila, Kwaya ya Kiinjilisti Kiranyi, Kwaya ya Habari Njema, Kwaya ya Amkeni Azimio, Daniel Ikoja, Upendo Kwaya na Ombeni Kwaya, na msherehashaji katika tukio hilo atakuwa ni Mc Elisha Mashauri.

Rose Mollel (Chipe) pia ameongeza kuwa atabarikiwa sana kuona kila mmoja anafika siku hiyo hasa kwa wakazi wa Arusha na mikoa yote ya jirani ambapo anaamini uzinduzi huo utakuwa baraka kwa kila mmoja atayefika siku hiyo hivyo amesisitiza watu wote wa rika zote, dini zote kufika siku hiyo na kwa wale ambao watashindwa kufika siku hiyo, baada ya uzinduzi huu album hizo zitaweza kuwafikia watu wote kuanzia Arusha na mikoa yote ya Tanzania kupitia mawakala mbalimbali wa usambazaji wa kazi za waimbaji wa nyimbo za Injili.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu uzinduzi wa album hizi na jinsi ya kuzipata nakala za album hizo wasiliana na muimbaji Rose Mollel (Chipe) Kupitia:

Simu/WhatsApp: +255759 085 181, +255 658 085 181, 255 764 107 111
Instagram: @rose_chipe
Facebook: Rose Chipe
Youtube: Rose Mollel

To Top