Connect with us

Video: Rose Chipe – Hakuna Kama Yesu

Muziki

Video: Rose Chipe – Hakuna Kama Yesu

Kutoka jijini Arusha leo tunaitambulisha kwako rasmi video mpya iitwayo Hakuna Kama Yesu kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Rose Chipe.

Video hii imeongozwa na director Joe kutoka studio za Amazing Pix Production, Muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Aflob chini ya mikono ya prodyuza Alex Lobulu.

“Nimeamua kuwaletea zawadi ya video hii kwa watu wa Mungu hasa katika majira haya ya kukumbuka kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo, Hakika hakuna aliye Kama Yesu kwasababu yeye ni mwokozi, ni rafiki, ni mtetezi wa watu wote. Naamini video hii itakwenda kubariki na kugusa moyo wako na hata wale ambao bado hawajajua thamani ya ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo basi wimbo huu ukapate kibali katika mioyo yao na kufunguliwa, Amen.” – alisema Rose Chipe.

Hakuna Kama Yesu ni moja kati nyimbo zinazopatikana katika album yake iitwayo Nimekutana na Yesu ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo 6 katika mfumo wa Audio CD.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki na kukuinua kila wakati utakapokuwa unaitazama, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Rose Chipe kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 621 077 670
Facebook: Rose Chipe
Instagram: @rose_chipe
Youtube: Rose Chipe

1 Comment

1 Comment

  1. Hornby

    December 24, 2018 at 1:30 am

    why doesnt it play?? Rose work on it please we love to listen to it

Leave a Reply

Your email address will not be published.

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top