Rose Chipe aja na zawadi ya kufunga mwaka - Gospo Media
Connect with us

Rose Chipe aja na zawadi ya kufunga mwaka

Habari

Rose Chipe aja na zawadi ya kufunga mwaka

Siku chache zijazo Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Arusha Rose Chipe anatarajia kuachia video yake mpya ya wimbo uitwao Hakuna Kama Yesu ikiwa ni baada ya kimya cha muda wa takribani mwaka mmoja toka alipoachia wimbo huo Juni 2017.

Video hiyo imeongozwa na director Joe kutoka studio za Amazing Pix Production, Muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Aflob chini ya mikono ya prodyuza Alex Lobulu.

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Rose Chipe alisema:

“Nimeamua kuwaletea zawadi ya video kwa watu wa Mungu katika majira haya ya kukumbuka kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo ndio maana nikasema Hakuna Aliye Kama Yesu, Ni mwokozi, ni rafiki, ni mtetezi wa wote bila ubaguzi. Naamini video hii itakwenda kubariki na kugusa mioyo ya watu wengi na hata wale ambao bado hawajajua thamani ya ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo katika maisha yao, Wimbo huu utakwenda kuwafungua na kuwa vumbe wapya.”

Mwimbaji Rose Chipe

Hakuna Kama Yesu ni moja ya wimbo unaopatikana katika album yake iitwayo Nimekutana na Yesu ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo 6 katika mfumo wa Audio CD.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Rose Chipe kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 621 077 670
Facebook: Rose Chipe
Instagram: @rose_chipe
Youtube: Rose Chipe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top