Habari

Rogate Kalengo wa GSS(2016)Dar Kufanya Uzinduzi wa Albamu yake April 23 Mwaka Huu.

Aliyewahi kuwa Mshindi wa tatu wa Gospel Star Search (Gss-2016) Rogate Kalengo anatarajia kufanya uzinduzi wa Albamu yake ya Kuna Namna mwishoni mwa  mwezi wa nne mwaka huu.

Akizungumza na Gospo Media alisema kuwa, maandalizi yote yapo katika hatua za mwisho mwisho ili kulifanya tamasha hilo kuwa la kipekee na la namna yake.

‘Kiukweli maandalizi ya uzinduzi wa albamu yangu ya Kuna Namna yamekamilika kwa upande wa mazoezi  na vyombo,ni kwa sehemu ndogo sana ambayo nayo nikishirikiana na watu wangu wa karibu tunaelekea kukamilisha ni kwa kumpata mgeni rasm wa siku hiyo pamoja na waimbaji watakao nisindikiza ama kunisapoti wakati wa uzinduzi wa albamu yangu pia nimesikia watu wameanza kuulizia nitafanyia wapi kwa maana ya ukumbi naomba kuwaambia watulie kwa sasa maana nimepata maeneo mengi, sasa ninachokifanya na kamati yangu ni kuchagua wapi tukafanyie uzinduzi na tukishapata mapema sana tutawataarifu wapenzi na wafuasi wa muziki wa injili ili waje siku hiyo tumsifu na kumtukuza Mungu”. Alisema Rogate Kalengo.

Mwimbaji huyo anayetamba kwa nyimbo zake mbili mpka sasa kama Kuna Namna pamoja na wimbo wake aliuachia juma moja lililopita uitwao Ombi Langu na ambao unafanya vyema mpaka sasa kwenye media mbalimbali hapa nchini.

Kwa mawasiliano na Rogate kalengo

Facebook: Rogate Kalengo

Instagram: @rogate-kalengo

Whatsapp and calls: +255(0)752 254 801.

YouTube: Rogate Kalengo
Email: rogatekalengo@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Mc Freddie Feat Mr.Mike-Wakusamehe

Next post

Mashabiki Nchini Kenya Wampendekeza Urban Settlah kuingia Groove Award Kama Mwimbaji Chipukizi.