Ritha Komba afanikisha uzinduzi wa Ni Rafiki kwa Kishindo - Gospo Media
Connect with us

Ritha Komba afanikisha uzinduzi wa Ni Rafiki kwa Kishindo

Matukio

Ritha Komba afanikisha uzinduzi wa Ni Rafiki kwa Kishindo

Siku ya tarehe 28 Oktoba 2018 mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania maarufu kama Ritha Komba amefanikiwa kuzindua rasmi albamu yake mpya iitwayo Ni Rafiki ikiwa katika mfumo wa Audio na Video.

Mwimbaji huyo tayari ameweza kufahamika katika huduma ya muziki wa Injili ndani na nje ya mipaka ya Afrika Mashariki kupitia nyimbo na video mbalimbali ambazo ameshaziachia na kufanya vizuri ikwemo Mungu wa Ajabu, Kivulini na Nitashinda

Mchungaji John Daimon (Mume wa Ritha Komba) wa huduma ya Eloi Center akizungumza Jambo katika uzinduzi wa albamu hiyo.

Akizungumza na Gospo Media Ritha Komba amesema kuwa anamshukuru Mungu sana kwa hatua hii ambayo amefikia kwa kuzindua albamu yake ya kwanza toka aanze huduma ya uimbaji wa nyimbo za Injili na hii imekuwa ni alama kubwa ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kufanikisha jambo hilo ambalo anasema lilikuwa kama ndoto iliyokuwa ikimtesa muda mrefu.

Mwimbaji Ritha Komba akifanya yake kwa ubora mkubwa.

Uzinduzi wa albamu hiyo umefanyika katika ukumbi wa Jumba la makumbusho ya Taifa Posta, Karibu na Chuo cha IFM huku ukisindikizwa na waimbaji mbalimbali walioalikwa siku hiyo na kufuatiwa na tukio maalumu lililotambulika kama “Start Where You are With What You Have”, ambapo mwimbaji Ritha Komba alizungumza na vijana juu kuwa na uvumilivu na Imani katika kuzifanikisha ndoto zao katika kila kitu wanachokifanya.

Albamu ya Ni Rafiki ikiwekwa Wakfu na Kuzinduliwa Rasmi.

Kwasasa albamu hiyo inapatikana kupitia kampuni maarufu ya usambazaji wa albamu za waimbaji wa muziki wa Injili inayofahamika kama Mbogo Production zinazopatikana jijini Dar es salam.

Moja kati ya Praise Team zilizosindikiza uzinduzi wa Albamu hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi na jinsi ya kuipata nakala ya albamu hii pia katika mfumo wa Audio CD na Video DVD wasiliana na mwimbaji Ritha Komba moja kwa moja kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook: Ritha Komba
Instagram: @rithakomba
Twittter: @rithakomba
Youtube: Ritha Komba

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Matukio

To Top