Habari

Ritha Awashukuru Wakazi wa Mkoa wa Morogoro Kwa Kuipokea Kivulini

Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Ritha Komba amewashukuru wakazi wa mkoa wa Morogoro na mikoa yote ya jirani kwa mapokezi mazuri juu ya kazi zake za nyimbo za Injili, hususani wimbo wake unaofahamika kwa jina la Kivulini.

Akizungumza kwa njia ya simu katika kipindi cha gospel cha Sua fm Ritha Komba alitoa shukrani kubwa huku akiwaomba washabiki zake kuendelea kusubiri kwani kuna ujio mpya wa kazi yake katikati ya mwezi wa kumi mwaka huu 2017.

Ritha Komba kwa sasa anatamba na wimbo wa Kivulini ambao tayari ameshaachia video na ni moja kati ya kazi inayoonekana kufanya vizuri katika mitandao ya kijamii, vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini.

Kama bado hujawahi kuizama video ya Kkivulini kutoka kwa mwanadada Ritha Komba tayari tumeksogezea hapa chini uweze kuitazama na kupakua wimbo huu na hakika utabarikiwa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ritha Komba kupitia
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook:
Ritha Komba
Instagram:
@rithakomba
Email:
rithakomba@yahoo.com au synyoritha@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Snoop Dogg Kuachia Projekti Ya Kwanza Ya Muziki wa Injili Akiwa na Fred Hammond.

Next post

Deitrick Haddon Aachia Video yake Mpya - Come By Here. Itazame Hapa.