Video | Audio: Ringtone Feat Ada - This Year - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Ringtone Feat Ada – This Year

Video

Video | Audio: Ringtone Feat Ada – This Year

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini kenya ameachia video yake mpya iitwayo ”This Year” ikiwa ni kazi yake ya kwanza kwa mwaka 2018, hii imekuja baada ya miezi sita iliyopita kuachia video iitwayo “Wacha Iwe” akiwa amemshirikisha mwimbaji nguli Gloria Muliro, na sasa amevuka mipaka mpaka Afrika Magharibi na kufanikiwa kufanya colabo kubwa kutoka kwa moja ya mwimbaji aliyefanikiwa zaidi kutoka nchini Nigeria anayefahamika kwa jina la Ada Ehi.

Ada ni mwimbaji wa kimataifa, mwenye rekodi ya kuwa mwimbaji ambaye amepata umaarufu mkubwa kitaifa na kimataifa kupitia nyimbo zake na video za muziki tangu alipoanza kazi ya muziki mwaka 2009.

Mnamo mwaka wa 2017, alikuwa miongoni mwa waimbaji waliotangazwa katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa nchini Nigeria”. Pia alishinda Tuzo za Groove 2017 kama Msanii Bora wa Afrika Magharibi wa Mwaka.

“This Year” ni wimbo unaotangaza ushindi na mambo mema ambayo Mungu atafanya katika maisha yetu mwaka huu. Wimbo huu  pia unatuhimiza tusiwe na wasiwasi kwa sababu Mungu ana mpango mzuri nasi na wakati wa mzuri wa kudhihirisha ahadi zake katika maisha yetu ni mwaka huu.

Muziki huu umetayarishwa na studio za 5 Star Music na video ikiwa imeongozwa na director kutoka Nigeria anayefahamika kwa jina la Lawrence Omo-Iyare.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utabarikiwa sana!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Ringtone kupitia:
Facebook: Ringtone Apoko
Instagram: @ringtoneapoko
Youtube: Ringtone Apoko

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Video

To Top