Video: Richie Kisukuli - Sikati Tamaa - Gospo Media
Connect with us

Video: Richie Kisukuli – Sikati Tamaa

Video

Video: Richie Kisukuli – Sikati Tamaa

Baada ya kufanya vizuri mwaka 2018 kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kama Richie Kisukuli ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Sikati Tamaa.

Video hii imeongozwa na director Hanzo, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Ebby Production.

Sikati tamaa ni wimbo wa uamsho na wenye kumpa mtu nguvu mpya ya kusimama na kufanya kwa upya kwa yale ambayo ameyakosea hasa kwa kuishi katika maisha ya dhambi.

Kuna nyakati dunia inaweza kukufanya ukose amani, furaha, upendo na hata ukafika mbali zaidi na kufikiri Mungu hayupo lakini kupitia wimbo huu mtumishi wa Mungu Richie Kisukuli anatukumbusha kuwa katika mapito yote Yesu pekee ndio jibu la shida na mahangaiko yetu.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii na hakika utabarikiwa, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi wa Mungu Richie Kisukuli kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 746 468 922
Instagram: @richiekisukuli
Youtube: Richie Kisukuli

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top