Video | Audio: Rhoda Shunashu - Salama - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Rhoda Shunashu – Salama

Audio

Video | Audio: Rhoda Shunashu – Salama

Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Rhoda Shunashu na hii ni video yake ya kwanza iitwayo Salama.

Video hii imeongozwa director anayefahamika kwa jina la Hypa Ibadah kutoka studio za Fx, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza Brian Komakoma.

“Lengo la kutunga wimbo huu lilikuwa ni ombi langu kwa Mungu kuwa Yeye ni Nuru yangu, Kiongozi wangu na Mlinzi wangu, Asafishe njia yangu ili niweze kutembea SALAMA kwani mikononi mwake nipo SALAMA.

Hata adui wakijipanga kupigana nami sitaogopa maana yeye yupo pamoja nami na mikononi mwake amenificha, kila asubuhi na wakati wake niuone ukuu wake.” – alisema Rhoda Shunashu

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki kila wakati utakapokuwa unaitazama na kusikiliza wimbo huu, Amen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Rhoda Shunashu kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 684 464 642
Facebook: Rhoda _Tz
Instagram: @rhodashunashu
Youtube: Rhoda Shunashu

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top