Habari

Raisi Magufuli ashiriki ibada ya jumapili ya matawi, kanisa la mtakatifu Peter

Na Mwandishi wetu,

Rais John Magufuli na mke wake Janeth wameshiriki ibada ya Jumapili ya matawi leo Machi 25 katika Kanisa Katoliki la mtakatifu Peters lililopo jijini Dar es salaam wakiwa pamoja na mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa.

Ibada ya Jumapili ya Matawi huadhimishwa wiki moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka, kila mwaka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Peters Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akishukuru baada ya kupokea Sakramenti takatifu wakati wa Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Peters Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipeana amani na Masista wa Kanisa Katoliki walipojumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Peters Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Peters Oysterbay jijini Dar es salaam leo Machi 25, 2018.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Umoja na amani ya Tanzania viko hatarini, maaskofu wa kilutheri waonya

Next post

Maaskofu KKKT watoa waraka mzito kwa Taifa la Tanzania