Connect with us

Video | Audio: Rafiki Gospel Singers – Milele

Video

Video | Audio: Rafiki Gospel Singers – Milele

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa mara ya kwanza nimekusogezea video nzuri ya sifa iitwayo Milele kutoka kwa kundi jipya la muziki wa Injili Tanzania linalofahamika kwa jina la Rafiki Gospel Singers, video hii imeongozwa na director Jackson Joaqim kutoka studio za Blessing na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Abba kutoka studio za Instincty Records.

Milele ni wimbo wa sifa unaomtukuza na kumsifu Mungu kwa ukuu wake, upendo wake na yote ambayo amatutendea katika maisha yetu Bwana Yesu ni mkuu sana anasatahili sifa na utukufu, Kama andiko linavyosema katika kitabu cha zaburi 113:2 “Jina lake litukuzwe, sasa na hata milele.”

Rafiki Gospel Singers ni kundi linalopatikana jijini Dar es salaam, linaloundwa na vijana watano ambao wameokoka na wamejidhatiti kumtumikia Mungu kwa njia ya muziki wa Injili huku wakiamini kuwa utakwenda kubadilisha maisha ya watu kwa kiwango kikubwa kiroho na kimwili na hii ikiwa ni video yao ya kwanza kuiachia kwa 2018 ikiwa imebeba ujumbe wa kumsifu.

Nina imani kuwa utafurahia kuitazama video hii ambayo imeandaliwa kwa ubunifu wa kipekee na wimbo huu utakwenda kukubariki na kukuinua kila wakati utakapokuwa unasikiliza, Mungu akubariki kila iitwapo leo kwa kila  utakapokuwa unasikiliza na kutazama video hii, Ameen.

Download Audio Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na kundi la Rafiki Gospel Singers kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 660 543, +255 715 709 415, +255 712 746 398
Facebook: Rafiki Gospel Singers
Instagram: @rafiki_gospel_singers
Twittter: @rafikigospel_
Youtube: Rafiki Gospel Singers group

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top