Habari

Radi yaua 16, 140 wajeruhiwa kanisani Rwanda.

Na Mwandishi wetu, KIGALI, Rwanda.

Watu 16 wameuawa nchini Rwanda na wengine 140 wamejeruhiwa kutokana na Radi zilizopiga kanisa moja la sabato linalofahamika kama Adventist Church lililopo kusini mwa nchi hiyo siku ya jumamosi ya wiki iliyopita.

“Baadhi ya waumini walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya karibu, ambapo wawili bado wana hali mbaya.”  – alisema Rose Mureshyankwano, Gavana wa mkoa. Alisema watu 17 kati ya wale waliojeruhiwa bado wapo hospitali na wengine tayari wamesharuhusiwa. Tukio hilo lilitokea pia Ijumaa ya wiki hiyo ambapo Radi ilipiga kundi la wanafunzi 18 na kuua mmoja. Oktoba ya mwaka uliopita, Radi iliua watu 18 katika sehemu mbalimbali za nchi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya usimamizi wa maafa na wakimbizi nchini Rwanda zinasema kuwa matukio ya ajali zinazotokana na Radi zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika nchi hiyo, ambayo ina mabonde na milima mingi, ambapo kila mwaka serikali ya nchi hiyo imekuwa inapokea takwimu ya vifo vya binadamu na mifugo vinavyotokana na Radi hizo, ambapo 2016 ziliuwa watu 30, kujeruhi watu 61 na kuua mifugo 48.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Paul Payne837 Feat. DJ Victor256 - Nakana

Next post

Papa Francis kutembelea mataifa ya baltic, Septemba 2018.