Connect with us

Audio: Prosperity Bothers – Mungu Wetu

Audio

Audio: Prosperity Bothers – Mungu Wetu

Prosperity Bothers ni kundi jipya la waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 wameachia wimbo uitwao Mungu Wetu, Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Home Town chini ya mikono ya prodyuza Elly Da Bway.

Mungu Wetu ni wimbo wa sifa na shukrani kwa Mungu, Katika maisha yetu leo wanadamu tumekuwa tunapitia nyakati zenye machungu na shida nyingi sana ikiwemo magonjwa, uchumi, migogoro, mafarakano na mambo mengine kama hayo lakini Mungu kwa upendo wake mkuu amekuwa akionekana katika maisha yetu na kututetea, Zaburi 66:8 Msifuni Mungu wetu, enyi mataifa yote; tangazeni sifa zake zipate kusikika.

Prosperity Brothes ni kundi la vijana watatu akiwemo Kelvin Bosco, Cosmas Bosco na Frank Bosco wakiwa ni ndugu wa damu moja walioamua kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji wa nyimbo za Injili, wakiongea na gospomedia.com wamesema kuwa wanatarajia kuendelea kuachia kazi nyingi kuanzia mwaka huu 2018 ambazo wanaamini kuwa zitawagusa na kuwainua watu kwa namna ya kipekee kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni hakika kuwa utabarikiwa na kufurahia wimbo huu mzuri kutoka kundi la Prosperity Brothers, Bwana Yesu asifiwe.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na kundi la Prosperity Brothers kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 717 342 232
Facebook: Prosperity Brothers
Instagram: @prosperity_brothers
Youtube: Prosperity Brothers

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top