Video

Music Video | Audio: Promise Ndonge – Vitumbua na Mchicha

 

Kutoka kibaha maili moja leo nimekusogezea video yenye ujumbe wa kipekee iitwayo Vitumbua na Mchicha kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Promise Dina Ndonge. video hii imeongozwa na studio yake iitwayo Promise Production.

Video hii ndio inayobeba jina la albamu yake ya DVD yenye mkusanyiko wa nyimbo 7 ambazo ni hakika utazifurahia na kubarikiwa kutokana na jumbe zinazopatikana kwenye albamu hii ambayo kwasasa ipo sokoni na kusambazwa na yeye mwenyewe kupitia lebo yake ya Promise Production.

Vitumbua na Mchicha ni wimbo wa pekee unaohamasisha watu kujishughulisha na kuacha uvivu na uetegemezi ili kuweza kupata mahitaji yao ya kilasiku na kuboresha maisha yao.

Akizungumza na gospomedia.com mwimbaji Promise Ndonge amesema ”Huu ni wimbo pekee ambao niliamua uwe ndio unaobeba jina albamu yangu ya DVD kwasababu ni wimbo ambao umebeba ujumbe mkubwa wa kuwahimiza watu wafanye kazi waache uvivu, kulalamika na kukaa kwenye vigenge au vijiwe ambavyo kwa namna moja ama nyingine husababisha migogoro ya mara kwa mara ndani ya ndoa zao na familia zao kwa ujumla.

Huu ni ujumbe ambao nimekusudia uwafikie watu wote wale walio wakristo na wale wasio wakristo ili kila mtu kwa nafasi yake afahamu kuwa Mungu hapendi watu wavivu anapenda watu wanaopenda kufanya kazi ili kutengeneza familia zao kuwa imara kiroho na kimwili. Ni maombi yangu kila mtanzania apate DVD ya albamu hii ya Vitumbua na Mchicha itakayowahamasisha watu wafanye kazi, wasikate tamaa na waache kukaa bure tu wabadilike.” – Alisema Promise Dina Ndonge.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakufunza na kukuhamasisha wewe ambaye una roho ya uvivu naamini baada ya kutazama video hii Yesu atakupa nguvu ya kupenda kufanya kazi kupiti roho mtakatifu… Amen.

Download Audio

Kama wewe ni kijana na huna kazi unaweza kumpigia Promise Dina Ndonge na atakusaidia kupata kitu cha kufanya.

Kwa mawasiliano zaidi, mialiko na jinsi ya kuipata albamu hii wasiliana na mwimbaji Promise Ndonge kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 715 622 699, +255 683 494 825
Facebook: Promise Ndonge
Instagram: @promisendonge
Youtube: Promise Ndonge

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Audio: Neema Mudosa - Hawawezi

Next post

Music Video | Audio: Mr.Seed Feat Size 8 - Simba wa Yudah