Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Audio: Prince of Heaven – Sitabaki Kama Nilivyo

Audio

Audio: Prince of Heaven – Sitabaki Kama Nilivyo

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu leo nimekuletea wimbo mzuri na wenye kukutia moyo uitwao “Sitabaki Kama Nilivyo” kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Prince of Heaven Sebastian, Muziki huu umetayaarishwa ndani ya studio za Winess Records chini ya mikono ya prodyuza Tony.

“Sitabaki Kama Nilivyo” ni wimbo unaobeba albamu yake mpya ambayo kwasasa tayari imeshakamilika. Akiongea na blog ya gospomedia.com mwimbaji Prince aliweka wazi ushuhuda wake kuhusiana na wimbo huu.

“Sitabaki kama Nilivyo ni wimbo unaogusa maisha yangu moja kwa moja ambapo kabla sijampokea Yesu nilikuwa namsaidia baba yangu uchawi kupindi hicho nilikuwa nipo shule na baada ya kuokoka baba yangu akanifukuza nyumbani na kutaka kuniua, Akaanza kunitafuta na mapanga ndipo nikakimbilia Dar es salaam na nikawa napita katika maisha magumu sana hapo ndipo nilipopata wimbo huu mwaka 2014. Kwa hiyo kwa wewe ambaye unaona mbele yako kuna giza hadi umeshindwa kuendelea kama unatafuta mtoto umeombewa sana, umeenda kwa waganga sana kama ni kazi umetafuta sana, kama ni mke au mume umetafuta sana lakini hujapata nakusihi leo rudi kwa Mungu umtegemee yeye amini hutabaki kama ulivyo kwa hayo yote unayoyapitia.” – Prince of Heaven

Ni imani yangu kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu ambao utagusa na kubadilisha maisha yako kuanzia sasa, Ameen.

 

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/04/Prince-of-Heaven-Sitabaki-kama-Nilivyo.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Prince of Heaven kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 746 748 550, +255 673033450
Facebook: Sebastian Eriakim
Instagram: @princeofheaven

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 10 ON GOSPOMEDIA

SUBSCRIBE

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 12,309 other subscribers

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top