Connect with us

Video | Audio: Preye Odede – Oshimiriatata

Video

Video | Audio: Preye Odede – Oshimiriatata

Kutoka nchini Nigeria leo nimekusogezea video nzuri ya ushuhuda iitwayo Oshimiriatata kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Preye Odede. Video ya wimbo huu imeongozwa na director Adasa Cookey na muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Prince Vibes.

Oshimiriatata ni wimbo aliouachia Februari 2017 ikiwa ni moja kati ya nyimbo zinazopatikana kwenye albamu yake mpya iitwayo READY aliyoiachia disemba 2017.

“Yesu anatualika kunywa maji ya uzima kutoka kwake kama chanzo cha uhai wetu Yohana 7:37, “Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalumu. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwangu anywe.”

Wimbo huu umeimbwa katika lugha ya Igbo inayozungumzwa kati ya moja ya makabila yaliyopo nchini Nigeria, “Oshimiri Atata ” maana yake ni (mto usiokauka) ukiwa ni wimbo wa ibada na wenye kutambua asili ya Mungu wakati wote na Yeye akiwa kama chanzo cha uhai wetu. Daima husaidia, hulinda na kufanya mengi zaidi ambayo macho yetu ya nyama hayawezi kuona.

Hata wakati ambao tunapoteza na kukata tamaa, Mungu huwa nasi kila wakati, wakati wowote unaweza kumwita na akajibu – Preye Odede.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii nzuri na kupakua wimbo huu ambao nina imani kuwa utakubariki na kukuinua sana!

Download Audio

Social Media
Facebook: Preye Odede
Instagram: @preyeodede
Twittter: @preyeodede
Youtube: Preye Odede

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top