Connect with us

Audio: Peter Mdoe – Asante

Audio

Audio: Peter Mdoe – Asante

Moja kati ya mwimbaji anayeendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania ni huyu hapa anayefahamika kwa jina la Peter Mdoe ambaye siku ya leo ameachia wimbo wake mpya wa shukrani uitwao Asante. Muziki huu umetayaarishwa ndani ya studio za Republic of Music chini ya mikono ya prodyuza Mpeula Msami.

Asante ni wimbo unaelezea upendo wa Mungu kwa jinsi unavyoweza kumtendea mtu ambaye amekuwa ni mkosefu mbele za Mungu lakini kwa upendo wake Mungu umemfanya kuwa mpya na leo anadhihirisha ushuhuda wake kupitia wimbo huu ambao unamrudishia Mungu shukurani kwa matendo yake makuu yaliyobadilisha maisha yake.

“Katika maisha tunapitia mengi yanayotufanya tumuache Mungu ila Mungu yeye hafikirii kutuacha kamwe, wengi wamepotea kenye ulevi na dhambi nyingi ila Mungu huwaepusha na matatizo juu ya hayo. Ukiona unapitia hayo na bado unadumu jiulize mara mbili mbili umemfanyia nini Mungu mpaka sasa ametuweka hai. Tunapaswa kujitakasa na kusema Ahsante kwa Mungu wetu kwa Upendo wake wa dhati anaotufanyia kutuepushia matatizo hata pale tunapomkosea.” – Alisema Peter Mdoe

Nina imani kuwa kupitia wimbo huu utabarikiwa na kubadilishwa na kama bado hujamkiri Yesu basi wimbo huu ukusaidie kumkabidhi Bwana maisha yako, Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Peter Mdoe kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 655 094 891
Facebook: Peter Mdoe
Instagram: @peter_mdoe

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top