Connect with us

Music Video | Audio: Paul Shole – Kibali

Video

Music Video | Audio: Paul Shole – Kibali

Shalom mwana wa Mungu! leo kwa mara ya nyingine tena nimekuletea video ya wimbo mzuri na wenye nguvu ya kukubariki uitwao Kibali kutoka kwa muimbji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili kutoka jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Paul Shole, video hii imeongozwa na director Robie One(Hero) na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za AB Records chini ya mikono ya prodyuza Elia.

gospomedia.com tulipata nafasi ya kuzungumza na mtumishi huyu wa Mungu Paul Shole kuhusiana na ujumbe ambao umekusudiwa katika wimbo huu na alikuwa na haya ya kusema:

”Nyimbo hii ya Kibali maana yake halisi ni kwamba kama tunamtumikia Mungu aliye hai lazima wewe kama muimbaji wa nyimbo za injili uwe na Kibali toka kwa yule aliyekupa Kibali yaani Mungu wetu yeye ndiye anayetoa Kibali, bila ya Kibali utakuwa unafanya kazi bure, Kibali pia kinawahusu hata wale ambao si waimbaji wanatumika kwenye mambo mengine kupitia wimbo huu pia nimewakumbusha kuwa Kibali ni kama ufunguo ambao Mungu hutoa kwa mtu kwa kusudi la kuitenda kazi yake na kuifanikisha hivyo ninachotaka kuwakumbusha watu wa Mungu hapa ni kwamba kila jambo tunalotaka kufanya ni lazima tumshirikishe Mungu na kupitia jina la Yesu Kristo tuweze kupata ruhusa ya kufanya yale ambayo Mungu amekusudia kwetu kutumia nguvu nyingi katika kutafuta mafanikio bila kumshirikisha Mungu huo ni ukaidi na kiburi mbele za Mungu.” – Alisema Paul Shole

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina imani utakubariki sana siku ya leo!! Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Paul Shole kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 752 764 360
Facebook: Paulo shole
Instagram: @pauloshole
YouTube: Paulo Shole
Twitter: @pauloshole

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Video

To Top