Habari

Papa Francis kutembelea mataifa ya baltic, Septemba 2018.

Vatican imesema Papa Francis atatembelea taifa la Lithuania, Latvia na Estonia mnamo Septemba 22-25 yakiwa ni mataifa matatu ya Baltic yanayosherehekea maadhimisho ya miaka 100 ya umoja wao. Vatican imethibitisha safari hiyo Ijumaa ya wiki iliyopita, wakisema Papa Francis atatembelea mji wa Vilnius na Kaunas huko Lithuania; Riga na Aglona huko Latvia, na Tallinn huko Estonia.

Lithuania ina jumuiya kubwa ya Kikatoliki katika mataifa ya Baltics, ikiwa na zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa nchi hizo ambayo sawa na karibu watu milioni 3.

Mataifa hayo matatu ya Baltic yalitangaza uhuru wao kutoka kwenye mikono ya Urusi mwaka wa 1918 lakini yaliingizwa katika Umoja wa Sovieti mwaka wa 1940 na ikawa sehemu yake mpaka 1991.

Kwa nafasi iliyobaki kwa mwaka 2018 Papa Francis ana safari nyingine moja tu iliyothibitishwa ambayo ni safari ya kuelekea Geneva mwezi Juni. Pia anatarajia kwenda Ireland mwezi Agosti kwa Mkutano wa Dunia unaohusu Familia.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Radi yaua 16, 140 wajeruhiwa kanisani Rwanda.

Next post

Video | Audio: Andrew Robinson - Ni Neema Yako